WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametangaza uamuzi wa Serikali wa kuondoa tozo 42
kati ya 47 ambazo walikuwa wanatozwa wakulima wa kahawa wa Mkoa wa
Kagera hadi kufikia tozo 5 tu ambazo itakuwa ni jumla ya Shilingi 267
kwa kila kilo ya kahawa, kutoka Shilingi 830 za awali.
Waziri
Mkuu ametoa maamuzi hayo kufuatia tume maalum aliyoiunda ili kupitia
utaratibu na mfumo wa uendeshaji wa vyama vya Ushirika wa zao la kahawa
Mkoani Kagera.
Mheshimiwa Majaliwa amewaagiza viongozi wa vyama
vya Ushirika, wasimamie vyama vyao kwa uaminifu na weledi ili vilete
tija kwa wakulima.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa amewata viongozi wa
vyama vikuu vya ushirika kuacha tabia ya kukopa pesa benki kwa ajili ya
kununua kahawa kwa wakulima.
Waziri Mkuu ameyatoa maagizo hayo
leo (Jumanne, Machi 29, 2022) Wakati alipoendesha Mkutano Maalum wa
Wadau wa zao la kahawa mkoani Kagera uliofanyika wilayani Karagwe Mkoa
wa Kagera.
Amesema kuanzia sasa mauzo ya kahawa katika Mkoa wa
Kagera yatafanyika kwa njia ya mnada. “Mnada huo utafanyika kwenye ngazi
ya vyama vya msingi.”
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema
baadhi ya vyama vya ushirika vimekuwa vikiwaumiza wakulima wa kahawa kwa
kuwaongezea tozo zisizokuwa na tija.
Amesema jambo hilo
linafanyiwa kazi kwani wakulima wa kahawa mkoani Kagera wamekuwa wakilia
na tozo kubwa zaidi ya 47 na bado wamekuwa wakicheleweshewa malipo.
Waziri
huyo amemuagiza Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa kugawa miche ya kutosha ya
kahawa kwa wakulima ili ilete tija na kuwaongezea kipato.
Amesema
ili kuhakikisha maafisa ugani wanatekeleza majukumu yao ipasavyo Wizara
imeandaa utaratibu wa kutoa usafiri pamoja na vifaa vya kupimia udongo.
Awali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora
alisema katika msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022 mkoa ulizalisha jumla
ya tani 52,000 za kahawa ya maganda iliyokuwa na thamani ya sh. bilioni
69.
“Bei ya kahawa imeendelea kuimarika kwani katika msimu huu
wakulimwa walilipwa shilingi elfu 1,300 kwa kilo moja ya kahawa ya
maganda na Shilingi elfu 3,300 kwa kilo moja ya kahawa hai (Organic
cofee).”
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Innocent
Bashungwa alisema kutokana na usimamizi mzuri wa Serikali ya awamu ya
sita katika zao la kahawa, tayari wakulima wemeanza kuona manufaa kwani
bei ya zao hilo imepanda.
Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Tume
Maalumu ya kuchunguza mwenendo wa zao hilo. Dkt. Fabian Magawa Madele,
alisema katika uchunguzi waligundua ubadhirifu wa zaidi ya shilingi
bilioni saba ambazo zilitumika nje ya utaratibu wa vyama vya Ushirika.
Wednesday, March 30, 2022

SERIKALI YAFUTA TOZO 42 ZAO LA KAHAWA-MAJALIWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment