Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro leo Machi 29 amekutana na
kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright
kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji
wa Wanyamapori
Katika mazungumzo hayo Waziri Dkt.Ndumbaro
amemueleza Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuweka mazingira rafiki
ya Uwekezaji kwa Wawekezaji wa kutoka Marekani hususani katika sekta ya
Uwindaji wa Kitalii kwa kuzingatia maslahi ya nchi
" Moja ya
shabaha yetu kama Wizara ni kuwavutia Wawekezaji, tunafanya kila
liwezekanalo ili kuhakikisha Wawekezaji wa kutoka nchi mbalimbali
wakiwemo wa Marekani wanawekeza katika uwekezaji huu wa muda mrefu''
amesisitiza Dkt. Ndumbaro
Wizara ya Maliasili na Utalii
inatarajia kukusanya Sh23 bilioni kwa mwaka kutokana na uwekezaji mahiri
unaoendekea kufanywa kwenye sekta ya utalii nchini
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), akiwa kwenye picha
ya pamoja mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani
Nchini, Dkt. Donald Wright kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri
katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori . Kikao hicho kimefanyika leo
Jijini Dar es Salaam Picha na WMU
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), akiagana na Balozi
wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright mara baada ya kufanya mazungumzo
kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya
Uwindaji wa Wanyamapori . Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dar es
Salaam Picha na WMU
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), akizungumza na
Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright kuhusu masuala mbalimbali
ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori . Kikao
hicho kimefanyika leo Jijini Dar es Salaam Picha na WMU
Wednesday, March 30, 2022

Home
HABARI
WAZIRI DKT. NDUMBARO ATETA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI, DKT. DONALD WRIGHT KUHUSU SWICA
WAZIRI DKT. NDUMBARO ATETA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI, DKT. DONALD WRIGHT KUHUSU SWICA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment