HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 8, 2022

SERIKALI YAANDAA MKAKATI MAGARI YA ABIRIA YAKAGULIWE NA NIT

Mkufunzi wa masuala ya Anga, Mhandisi Sakawa Shungu akitoa maelekezo kwa Naibu Katibu Mkuu-Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Ally Possi wakati alipofanya ziara katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo jijini Dar es Salaam.

 

Mkaguzi wa Magari wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mtatiro Boniphace akitoa maelezo ya kifaa moja wapo cha kukagulia magari leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu-Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Ally Possi.
Naibu Katibu Mkuu-Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Ally Possi  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT leo Februari 8, 2022 jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT, profesa Zacharia Mganilwa .
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT, profesa Zacharia Mganilwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaa wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu-Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Ally Possi.  
Mkaguzi wa Magari wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Elias Shoki akitoa maelezo ya kifaa moja wapo cha kukagulia magari leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu-Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Ally Possi.
Mkuu wa Kituo cha kukagulia magari, Mhandisi Christian Nabora mwenye shati jeupe akitoa maelezo ya kifaa moja wapo cha kukagulia magari leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu-Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Ally Possi.

Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii
SERIKALI inaandaa mkakati wa kuwashauri wamiriki wa magari ya abiria yaendayo mikoani yawe yanapelekwa kwanza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kwa ajili ya ukaguzi na matengenezo ili yawe salama na kupunguza ajali.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu-Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Ally Possi wakati alipomaliza kutembelea Chuo hicho kwa lengo la kutambua kazi zinazofanywa na NIT leo Februari 8, 2022 jijini Dar Es Salaam.

"Moja ya changamoto ambazo zipo katika miji mikubwa hususani Dar es Salaam ni kutokea kwa ajali za barabarani kwa hiyo kunahaja ya kituo cha ukaguzi wa Magari kilichopo NIT kutumika kwaajili kukagua magari ya abiria. Amesema Possi.

Amesema NIT inafanya kazi nzuri ya kukagua vyombo vya usafiri na kuhakikisha vipo katika hali salama, hivyo ni vema wananchi wakajua kazi hiyo inayofanywa na chuo hiki ili kuhakikisha tunakuwa na vyombo salama vya usafiri

"Kazi nzuri tumeiona ni NIT kukagua vyombo na kuhakikisha vipo katika hali salama, moja ya maelekezo niliyotoa kwa chuo ni kuhakikisha wananachi wanajua kazi inayofanywa na Chuo... kama mlivyoona kuna vifaa vya kisasa ambavyo kila mwananchi akileta chombo chake kitakuwa salama." Amesema Dkt. Possi

Amesema Kuna mambo matatu ambayo kwa sasa Serikali inasimamia kwa spidi kubwa ikiwa ni pamoja na ukuzaji na uendelezaji wa shirika la ndege nchini.

Amesema kuwa changamoto kubwa ambayo nchi yetu inayo ni kukosa wataalamu wa kutosha siyo tu marubani.

Hata hivyo amewashauri NIT kuhakikisha wanatoa marubani na wataalamu wa ndege wa kutosha ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Ameongeza kuwa chuo hicho mwishoni mwa mwaka huu kinatarajia kupokea ndege mbili zenye thamani ya Sh. Bilioni tisa ambazo zitasaidia katika mafunzo ya anga kwa vitendo.

"Lakini pia kuna mradi mkubwa wa Standard geuge (SGR) ambao unahitaji wataalamu siyo tu madereva wa treni, wanatakiwa kuwepo wataalam ambao wanatakiwa kurekebisha hizo treni na mambo mengi katika mradi huo kwa ujumla." Amesema Dkt. Possi

Mbali ya miradi hiyo Dkt. Possi amesema kuna bandari ambayo ni kitovu cha uchumi nchi yetu lakini pia ni chanzo cha uchumi mpana upande wa SADC, hivyo wanahitaji wataalamu wa meli, wajengaji wa meli wasanifu meli, ambao wote wanatarajiwa kutoka chuo cha NIT.

Hata hivyo amechukua fursa ya kuwakaribisha wabunifu yoyote anatakiwa kupata utaalamu zaidi NIT.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT, profesa Zacharia Mganilwa amsema Chuo kinaendelea kutoa mafunzo ya utaalamu katika sekta mbalimbali ambapo katika kupanua wigo wa mafunzo wamepata eneo la ekari 125 mkoani Lindi ambapo baada ya kumaliza ujenzi wake watahamishia mafunzo mengine mkoani humo ambayo yamekwishaanza.

"Mpaka sasa kuna mafunzo ambayo yameanzia hapa kwa awamu ya kwanza lakini tutakapopata fedha za kuweza kujenga cumps Lindi tutahamishis wengine huko ili waweze kujitanua na baadae Tanzania iweze kuchukua soko la Afrika Mashariki yote." Amesema Profesa Mganilwa

Aidha profesa Mganilwa amesema, mwaka ujao Chuo kitapata wahitimu, kutokana na kozi ya Diploma in pipework Oil and Gas engineering ambapo wataalamu hao watakapohitimu wataweza kufanya mitihani ya Kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad