KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA KIPINDI CHA NUSU MWAKA JULAI HADI DESEMBA 2021 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 10, 2022

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA KIPINDI CHA NUSU MWAKA JULAI HADI DESEMBA 2021

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kipindi cha nusu mwaka, Februari 9, 2022 Jijini Dodoma.

Ofisi ya Waziri Mkuu imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi cha nusu mwaka Julai hadi Desemba 2021 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.

 

Kikao hicho kilihusisha Viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu akiwemo Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Dkt. Balozi Pindi Chana, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Jamal Katundu, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu pamoja na Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo. 

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia kikao cha kamati hiyo katika ukumbi wa Bunge, Februari 9, 2022 Jijini Dodoma.

Mwenyekiti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Najma Gigga (kushoto) wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa katika kikao cha kamati hiyo hii leo Februari 9, 2022 Jijini Dodoma.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Dkt. Balozi Pindi Chana akifafanua jambo katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kipindi cha nusu mwaka, Februari 9, 2022 Jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria iliyofanyika katika ukumbi wa Bunge, Februari 9, 2022 Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akieleza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Bunge, Februari 9, 2022 Jijini Dodoma.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kushoto), Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Dkt. Balozi Pindi Chana (katikati) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga wakifuatilia hoja iliyowasilishwa na Mwenyekiti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akieleza jambo katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kipindi cha nusu mwaka.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Jamal Katundu akieleza jambo katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kipindi cha nusu mwaka kilichofanyika katika ukumbi wa Bunge, Februari 9, 2022 Jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad