BENKI YA CRDB YAMKABIDHI MSHINDI WA BSS KITITA CHAKE CHA MILIONI 10 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 10, 2022

BENKI YA CRDB YAMKABIDHI MSHINDI WA BSS KITITA CHAKE CHA MILIONI 10

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi (Head of Consumer Banking), Stephen Adili (wa pili kushoto) akimkabidhi Mshindi wa BSS 2021 (Bongo Star Search), Yohana Braison Mwayinga, kitita cha shilingi milioni kumi (10,000,000/-) ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza, katika hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo kwenye tawi la Benki ya CRDB la Azikiwe, jijini Dar es salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BenchMark ambao ndio waendeshaji wa Mashindano ya BSS, Ritha Paulsen na kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe, Hamis Saleh.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Stephen Adili (kushoto) akimzungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Mshindi wa BSS 2021 (Bongo Star Search), Yohana Braison Mwayinga, kitita cha shilingi milioni kumi (10,000,000/-) ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza, iliyofanyika leo kwenye tawi la Benki ya CRDB la Azikiwe, jijini Dar es salaam. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BenchMark ambao ndio waendeshaji wa Mashindano ya BSS, Ritha Paulsen

Mshindi wa BSS 2021 (Bongo Star Search), Yohana Braison Mwayinga akizungumza.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi (Head of Consumer Banking), Stephen Adili (kushoto) pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe, Hamis Saleh (kulia) wakifurahia jambo baada ya kukabidi zawadi kwa washindi wa BSS 2021, Yohana Braison Mwayinga (mshindi wa kwanza), Andrew Charles Magalata (mshindi wa pili), Suleiya Abdi Abdillah (msindi wa tatu) wakiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BenchMark ambao ndio waendeshaji wa Mashindano ya BSS, Ritha Paulsen. hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo kwenye tawi la Benki ya CRDB la Azikiwe, jijini Dar es salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad