HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 9, 2022

MRISHO MPOTO ALAMBA DODO ,ATUMA SALAMU KWA WANAOMBEZA

Na Humphrey Shao, Michuzi TV

 MSANII wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ amewataka wasanii wa muziki kuacha kudharau aina ya uimbaji anaofanya kwani unampa dili nono.

Akizungumza Dar es Salaam jana,wakati akitia saini mkataba wa ubalozi wa miaka mitatu na kampuni ya Jatu PLC, Mpoto alisema wasanii wanapaswa kutumia sanaa kutangaza mambo mazuri yanayofanywa na serikali na kuacha kulalamika.

“Nashangaa wasanii wanasema kuwa mimi siimbi eti naongea, kupitia sanaa yangu hii leo nimekuwa balozi wa sekta ya maji,” alisema.

Alisema kupitia fursa hiyo atatumia kutangaza mambo mazuri yanayofanywa na serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Serikali hii ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kupeleka maendeleo na kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa juu, mambo makubwa rais anafanya lakini hayasimuliwi mimi nitatangaza hayo mambo,” alisema.


Mpoto aliteuliwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, kuwa balozi wa sekta ya maji Februari 7, mwaka huu,hatua hiyo ilikuja muda mchache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kusifu umahiri wake wa kukariri gharama za miradi ya maji na kuzitamka, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa maji wa Bunda mkoani Mara.

MSANII wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’  akibadilishana mkataba na Meneja wa Jatu Plc mara baada ya kumsaimisha mkataba wa miaka mitatu
MSANII wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’  akisaini Mkataba wa Miaka Mitatu na Kampuni ya Jatu Plc


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad