HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 3, 2022

BENKI YATOA MSAADA WA MADARASA NA MADAWATI SHULE SEKONDARI MASHUJAA

Mkuu wa Wilaya Ubungo, Kheri James (watatu kulia), Meneja Mwandamizi wa Uwekezaji kwa Jamii wa Benki ya CRDB, Joyceline Makule (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mashujaa, Prof. Alphonce Kyessi kwa pamoja wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa udhamini wa Benki ya CRDB pamoja na madawati 125, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni hamsini (50,000,000/-), katika hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika leo kwenye Shule hiyo, iliyopo eneo la Sinza B, Dar es salaam. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri wa Ubungo, Dkt. Peter Nsanya (katikati), Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sinza B, Said Hamza pamoja na Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Zawadi Rashid.
Mkuu wa Wilaya Ubungo, Kheri James akifurahi jambo na mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mashujaa, wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa udhamini wa Benki ya CRDB pamoja na madawati 125, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni hamsini (50,000,000/-) iliyofanyika leo kwenye Shule hiyo, iliyopo eneo la Sinza B, Dar es salaam. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa Uwekezaji kwa Jamii wa Benki ya CRDB, Joyceline Makule na Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mashujaa, Prof. Alphonce Kyessi.
Mkuu wa Wilaya Ubungo, Kheri James akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mashujaa, Prof. Alphonce Kyessi wakati wakiwa katika moja ya madarasa mawili yaliyojengwa kwa udhamini wa Benki ya CRDB pamoja na madawati 125, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni hamsini (50,000,000/-); wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kwenye Shule hiyo, iliyopo eneo la Sinza B, Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Uwekezaji kwa Jamii wa Benki ya CRDB, Joyceline Makule.
Mkuu wa Wilaya Ubungo, Kheri James (kushoto) akishuhudia tukio la kukabidhi cheti lililofanywa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Mashujaa, Mwalimu Zawadi Rashid (kulia) kwa Meneja Mwandamizi wa Uwekezaji kwa Jamii wa Benki ya CRDB, Joyceline Makule ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa Benki CRDB katika shule hiyo, katika hafla ya ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa udhamini wa Benki hiyo iliyokwenda sambamba na utoaji wa madawati 125, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni hamsini (50,000,000/-) iliyofanyika leo kwenye Shule hiyo, iliyopo eneo la Sinza B, Dar es salaam. 
Mkuu wa Wilaya Ubungo, Kheri James akizungumza katika hafla hiyo.
Meneja Mwandamizi wa Uwekezaji kwa Jamii wa Benki ya CRDB, Joyceline Makule akizungumza katika hafla hiyo.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad