ST BONGO NA STARTIMES WAJA NA THE BEST COMEDY CHALLENGE. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 4, 2022

ST BONGO NA STARTIMES WAJA NA THE BEST COMEDY CHALLENGE.

Na.Khadija Seif,Michuzi TV

VIJANA watakiwa kutumia talanta zao kama chachu ya kujipatia kipato na kuwaaminisha watu kuwa ni sehemu Moja ya kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza hayo Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malissa amesema Vijana wengi wamekua na talanta mbalimbali hivyo kupitia Kampuni hiyo inaendeleza mchakato huo kuona Kwa jinsi gani vijana wanatimiza ndoto zao.

"Kupitia Startimes tuliweza kubuni Mashindano mbalimbali ikiwemo "Bingwa show" ambapo ilikusanya vijana wenye umaarufu kupitia Mitandao ya kijamii na Mshindi aliweza kujinyakulia gari mpya na licha ya hivyo Kwa dhati tuliona vijana bado wanahitaji vipindi ambavyo kwao itakua ni mchongo tukadondosha Tena "Mr right" hivyo basi Kwa kupitia talanta zao zinawawezesha kupata au kutimiza ndoto za Maisha Yao kumiliki gari za kifahari pamoja na pesa taslimu."

Hata hivyo Malissa ameongeza kuwa Kwa kushirikiana na Mchekeshaji maarufu nchini "coy mzungu " wametambulisha Shindano jipya "The best comedy challenge" kupitia televisheni mpya ndani ya king'amuzi Cha startimes st bongo  chaneli 141.

Aidha Mkurugenzi wa Biashara na Mikakati wa televisheni Stbongo Isaya Kandonga aeleza namna televisheni hiyo imejikita zaidi kwenye Maudhui ya Filamu na Reality show.

"The comedy challenge unakuja kuvunja mbavu watu hivyo ningependa watazame show hiyo inayobadilisha Maisha ya vijana wenye vipaji vya kuvunja mbavu watu na itaruka muda mzuri ambao watu wameshatoka makazini."

Pia amesema kipindi hiko kitaanza kuruka rasmi Februari 6 kupitia chaneli 141 kuanzia saa 3 usiku .Kwa upande wake Coy mzungu amesema kuwa Startimes wanaendelea kuthamini vijana hivyo wachekeshaji hao watumie nafasi hiyo ya kujitangaza na kukamilsha ndoto zao.

"Fursa ya uchekeshaji ni Miongoni mwa fursa zinazoleta kipato hivyo Kampuni ya Startimes imelibeba jukumu hilo na linaenda kuvadilisha taswira na Mapinduzi katika tasnia hii Kwa kupitia Shindano la "The best comedy challenge".

Aidha ameweka wazi kuwa Shindano hilo litafanyika kupitia televisheni  ya st bongo na washiriki wataweza kupigiwa kura Kwa njia ya Mtandao "startimes on" na Mshindi wa kwanza atajinyakulia gari aina ya "crown" na Mshindi wa pili atapatiwa pesa shilingi Milioni 5, Huku Mshindi wa 3 atapatiwa kufuta Jasho shilingi Milioni 3.


Coy amefafanua zaidi kipengele kingine ni Mchekeshaji anaependwa na watazamaji ataweza kujipatia shilingi Milioni 1 kama zawadi.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malissa akifafanua baada ya kuzindua kipindi kipya "The best comedy challenge, na amegusia  zaidi namna Kampuni hiyo ilivyojikita katika kuwaibua vijana katika kutumia talanta zao kama njia ya kujipatia kipato na kubadilisha Maisha 

 Mchekeshaji maarufu nchini Coy Mzungu akitaja zawadi Kwa washindi watakazopatiwa kupitia kipindi kipya "The best comedy challenge" kitakachoanza rasmi Februari 6 mwaka huu kupitia chaneli 141 St bongo kupitia Kingamuzi cha Startimes

Mkurugenzi wa Biashara na Mikakati wa televisheni mpya ya St bongo Isaya Kandonga akifafanua zaidi kwa namna televisheni hiyo ilivyojikita Katika kutangaza Maudhui ya Filamu na Reality show

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad