WADAU KUPANDA MITI ZAIDI YA 2000 KUUNGA MKONO KAMPENI YA RC MAKALLA " SAFISHA PENDEZESHA DSM" - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 31, 2022

WADAU KUPANDA MITI ZAIDI YA 2000 KUUNGA MKONO KAMPENI YA RC MAKALLA " SAFISHA PENDEZESHA DSM"


Na Mwandishi Wetu

Ikiwa ni muendelezo wa Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM tangu kuzinduliwa rasmi na RC Makalla  ameungana na wakazi wa Manzese Manispaa ya Ubungo kufanya usafi, huku akiwapongeza kwa kujumuika naye katika zoezi hilo.


RC Makalla ametoa wito kwa Wakazi wa DSM kuendelea kufanya usafi ili Jiji liwe safi kwa kuwa DSM ndio lango la Tanzania, Vilevile amesema wafanyabiashara wadogo wasirudi tena Barabarani kwa kuwa kufanya biashara holela ni chanzo kikubwa cha Uchafu. 


Katika kuunga mkono juhudi hizo za RC Makalla Kampuni ya Mondi LTD ambao wanajishughulisha na Usafi wa mito, kutoa taka ngumu na tope na mchanga ambao unatumika kwa Ujenzi leo wameunguna na Mkuu wa Mkoa wa DSM kufanya usafi na kupanda miti katika mto Mpigi Bunju B.


Akiongea wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bwana Francis Mondi amesema pamoja na shughuli za kila siku za Kampuni hiyo leo Januari 29, wameunguna na RC Makalla kufanya usafi na kupanda miti, leo wamepanda 500 wataendelea kupanda, huku akiahidi kuendelea kuunga mkono Kampeni mbalimbali katika Mkoa wa DSM


Aidha Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu Mkoa Dkt Elizabeth Mshote amewashukuru wadau kwa kushiriki kupanda miti na kuienzi kwa vitendo Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DSM pia kubuni wazo la kuwa na kitalu katika eneo la Bunju B ambacho kitasaidia kuzalisha miche ya miti ambayo itapandwa katika maeneo mengine ya Mkoa wa DSM


Ifahamike kuwa leo Januari 29,2022 ni mwisho wa mwezi ambapo kufuatia agizo la RC Makalla Wakazi wa Dar es Salaam wameshiriki kufanya usafi wa pamoja katika maeneo yao pamoja na kupanda miti Zoezi hili ni endelevu likisimamia nguzo kuu nne; Kuwapanga wafanya biashara vizuri; Kufanya usafi; Kuboresha mazingira ya wafanyabiashara; Kuhakikisha wafanyabiashara hawarudi katika maeneo waliyoondolewa

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu Mkoa Dkt Elizabeth Mshote akipanda miti kando kando mwa Mto Mpiji
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bwana Francis Mondi akipanda mti kama ishara ya kuunga mkono kampeni ya Usafi ya Pendezesha Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad