UVCCM MBEZI WAANZA KUSHEREHEKEA MIAKA 46 YA CCM - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 31, 2022

UVCCM MBEZI WAANZA KUSHEREHEKEA MIAKA 46 YA CCM

 

Na Khadija Kalili
WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Makabe Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam wameishukuru serikali kwa kuelekeza fedha katika miradi mbalimbali ya elimu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Wakizungumza wakati wa ziara shuleni hapo iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mbezi Wilaya ya Ubungo ikiwa ni katika kuelekea kile cha maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama hicho inayoadhimishwa Kila ifikapo Februari 5 kila mwaka.

UVCCM Kata ya Mbezi iliyolenga kutembelea kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile inayojengwa kupitia fedha za miradi ya maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii, wanafunzi hao wamesema ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea nchi nzima umekuwa mkombozi kwa wanafunzi.

Mwenyekiti wa UVCCM Mary Bitta amesema kuwa wametembelea Shule hiyo ya Sekondari na kuona namna ahadi za Chama zikiwa zimetekelezwa ipasavyo.

Wakati huohuo wanafunzi wa kidato Cha kwanza shuleni hapo Lewis Nyoni na Caroline Matagogwa wote kwa pamoja walitoa neno la shukran kwa niaba ya wanafunzi wenzao huku walisema kuwa wanashukuru serikali ya wamu ya sita kwa kuwajengea Shule hiyo jambo ambalo limechangia wao kutokwenda kusoma mbali na maeneo ya makazi Yao huku wakiahidi kusoma kwa bidii Ili waweze kuzifikia ndoto zao.

Katika ziiara ya hiyo ya UVCCM Kata ya mbezi , ilihusisha makada mbalimbali kutoka katika kata za jirani pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Mbezi Othman Shaibu

Mwenyekiti wa UVCCM Bitta ameeleza kuwa mbali na kufanya ziara ya kutembelea Shule ya Sekondari Makabe miradi mingine ambayo waliitembelea ni pamoja na Kituo kikubwa Cha Mabasi yaendayo Mikoani (Magufuli Bus Stand) ,pamoja na mradi wa kitalu darasa uliopo Mabwepande ambapo kilijemgwa na Vijana 20 huku wengine 80 wKitarajiwa kuja kjiunga kwa ajili ya kupata mafunzo ya namna ya kupanda mazao na kitatunza takiwa ndani ya kitalu hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad