Taasisi ya
Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), iliandaa Kongamano la Fursa za Uwekezaji
na Biashara lililofanyika katika ofisi za Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es
Salaam, ikiwa na lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali katika sekta za
kilimo, ufugaji, teknolojia, upatikanaji wa mitaji na masoko.
Akizungumza
wakati wa kufungua Kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa (ESRF) Dkt. Tausi
Kida alisema, wataalam mbalimbali watawasilisha mada katika fursa ambazo
zimefanyiwa tafiti za kina na Taasisi hiyo ambapo mada hizo zimegawanyika
katika maeneo makuu manne ambayo ni: (1)Fursa zilizopo katika sekta mbalimbali
katika mikoa hapa nchini, (2)Fursa katika Teknolojia, (3)Fursa ya upatikanaji
wa masoko pamoja na (4) Namna ya kupata mitaji.
Dkt. Tausi
alifafanua kwamba, fursa zitakazozungumziwa katika kongamano hili zitajikita
katika sekta mbali mbali ikiwemo kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii, madini,
viwanda, usafirishaji, ujenzi, afya na elimu. Aidha, alisema kuwa kutakuwa na
mawasilisho yatakayojikita kwenye fursa mbalimbali katika kilimo biashara
(Agribusiness) kama vile Kilimo cha mbogamboga bila kutumia udongo (Hydroponic
vegetable), Kilimo cha malisho ya mifugo bila kutumia udongo(Hydroponic fodder),
kilimo katika shamba kitalu (Green House), ufugaji wa samaki katika vizimba
(cage) katika mabwawa (ponds), katika matanki (RAS), ufugaji wa kisasa wa nyuki
ikiambatana na shuhuda kutoka kwa wadau mbalimbali wanaofanya Kilimo Biashara
kwa tija.
Kwa upande
wa upatikanaji wa mitaji, Dkt. Kida alisema kuwa, wafanyabiashara wengi pamoja
na wakulima wanapata changamoto kwenye upatikanaji wa mitaji ambapo wengi
hawajui namna ya kuweza kupata mitaji au uelewa wa namna ya kupata mitaji,
hivyo basi tutakuwa na wataalamu kutoka mabenki na huduma nyingine za utoaji wa
mitaji ya kuleta maendeleo kwa watu na taifa kwa ujumla.
Aliongeza
kuwa kukua kwa sekta ya teknolojia duniani, sekta zote za maendeleo zinahitaji
matumizi ya teknolojia ili kufanya shughuli zake kwa uharaka, uhakika na
ufanisi mkubwa ambao utaleta tija. Kwa kuliona hilo tumewaalika wataalamu ambao
leo hii watatoa mada juu ya matumizi ya teknolojia na jinsi teknolojia
inavyotumika katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Lakini pia tutakuwa na shuhuda mbalimbali za matumizi ya teknolojia kutoka kwa
wadau wanaofanya vyema katika shughuli zao, alisema Dkt. Kida.
Aidha, Dkt.
Kida alisisitiza kuwa, Fursa zilizopo hapa nchini ni nyingi sana kwani kila
mkoa wa Tanzania una fusra zake na hasa kwenye kilimo, ufugaji, madini na sekta
nyingine, hivyo amewaasa vijana kuchangamkia fursa hizo ili kujikwamua
kiuchumi.
Akitoa neno kwa
niaba ya Wizara ya Kilimo, Kaimu Mkurugenzi wa Kilimo upande wa Sera na Mipango
ndugu Gungu Mibavu, alisema serikali iko bega kwa bega na wadau wote wa Kilimo
kwa kuimarisha shughuli za ugani pamoja na kupunguza ama kuondoa kodi na tozo
mbalimbali ambazo zimekuwa kero kwa wadau wa Kilimo.
Akizungumzia
fursa mbalimbali katika upatikanaji wa masoko ya kuuza bidhaa, mwakilishi wa TANTRADE
Bw. John Fwalo alisema, Taasisi yao imekuwa ikitoa huduma mbalimbali kwa
wazalishaji wa bidhaa hapa nchini katika kuwatafutia masoko ya uhakika ndani na
nje ya nchi. Bw. Fwalo alitoa wito kuwa, TANTRADE wapo kuwasaidia wote ambao
watahitaji msaada wao katika upatikanaji wa masoko.
Aidha, mwakilishi wa taasisi ya PASS Bw. Hamisi Mmomi alisema, PASS hutoa
mikopo kwa wateja ambao wanazo dhamana na endepo mteja ana dhamana ya kiasi
kidogo wao wako tayari kumdhamini ili aweze kukopesheka.
Wadau
walioshiriki kwenye kongamano hilo ni Wizara ya Kilimo, Wizara ya Uwekezaji,
Viwanda na Biashara, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT), Aquaculture Association of Tanzania, Big Fish, Agriculture Media Ltd,
Green Fish Investment, Nyanzobe Ltd, IMADS, Tanganyika Apicultural Ltd, Shirika
la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO), Multics Company, Kampuni ya Ramani, Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), CRDB, TADB, SELF, PASS Trust na pamoja
na wadau wengine mbalimbali.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akitoa hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Fursa za Uwekezaji na
Biashara lililofanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar
es Salaam.
Dkt.
Daniel Ngowi Mshauri elekezi (ESRF) akizungumzia fursa mbalimbali za
kibiashara na uwekezaji zilizopo katika mikoa mbalimbali nchini wakati
wa Kongamano hilo.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Kilimo, Bwana Gungu Mibavu
akizungumza kuhusu namna serikali ilivyojipanga kuwasaidia wakulima
pamoja na wafugaji ikiwa ni pamoja na kuwaondolea vikwazo mbalimbali ili
kuweza kuongeza pato la Taifa wakati wa Kongamano la fursa za Uwekezaji
na Biashara lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo jijini
Dar es Salaam
Meja
Kelvin Ngondo Kutoka Jeshi la KujengaTaifa (JKT) akizungumza kuhusu
Kilimo Biaishara hasa kwenye Ufugaji wa samaki kisasa kwa kutumia
Vizimba, Matanki na mabwawa wakati wa Kongamano la fursa za Uwekezaji
na Biashara lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo jijini
Dar es SalaamMr.
Raphael Majivu Kutoka Agriculture Media Ltd akitoa mada kuhusu kilimo
cha kisasa cha chakula cha mifugo bila kutumia udongo (Hydroponic
Fodder & Azolla) wakati wa Kongamano la fursa za Uwekezaji na
Biashara lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo jijini Dar
es Salaam
Afisa
Mipango na Uwekezaji kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO),
Johari Masengi akitoa mada kuhusu fursa zilizopo katika Shirika hilo ili
kukuza Biashara na Uwekezaji kwa wafanyabishara wadogo wakati wa
Kongamano la fursa za Uwekezaji na Biashara lililofanyika katika ofisi
za taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Philemon
Kiemi Kutoka Tanganyika Apicultural Ltd akitoa mada kuhusu fursa
zilizipo katika Ufugaji wa kisasa wa nyuki pamoja na bidhaa mbalimbali
za nyuki wakati wa Kongamano la fursa za Uwekezaji na Biashara
lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Ian Usiri Kutoka ya Ramani akitoa mada kuhusu fursa za Kibiashara na
Uwekezaji kidigitali zinavyoweza kuongeza kipato pamoja na namna
unavyoweza kufanya kazi za kimtandao wakati wa Kongamano la fursa za
Uwekezaji na Biashara lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa Kilimo na Ufugaji waki fuatilia mada
mbalimbali kwenye Kongamano la fursa za Uwekezaji na Biashara
lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
lililofanyiaka katika ofisi za Taasisi hiyo Dar es Salaam.

lililofanyiaka katika ofisi za Taasisi hiyo Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment