CRB yataka makandarasi watumie mafunzo kuboresha kazi zao - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 29, 2022

CRB yataka makandarasi watumie mafunzo kuboresha kazi zao


Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB), Injinia Consolata Ngimbwa kulia akinakili jambo kutoka kwa mmoja wa washiriki wa mafunzo ya siku tatu kwa makandarasi wazalendo alipokuwa akitoa mchango wake kwenye mafunzo hayo. Katikati ni .         Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) QS Joseph Tango na kushoto ni Mratibu wa Mafunzo wa CRB, Msanifu Majengo, Neema Fuime Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MAKANDARASI nchini wametakiwa kuzingatia mafunzo wanayopata kwa kuhakikisha wanayatumia kuboresha kazi zao wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi.

Hayo yamesewa leo Januari 29, 2022 mkoani Dodoma na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi, Injinia Consolata Ngimbwa wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa makandarasi wazawa.

Amesema CRB imejitahidi kuandaa mafunzo mengi yakiwemo ya namna ya kuandaa mikataba, kujaza zabuni kielektroniki na namna ya kuwasilisha zabuni hivyo lazima makandarasi wayatumie kuongeza ubora wa kazi zao.

“Kuna mtu anachangia mada kwenye mkutano lakini akitoka hapo getini yote aliyojifunza anayaacha hapo sasa naomba tuyaishi haya tunayojifunza kwasababu ni kwa faida yetu sisi wenyewe kukuza biashara hii. Mwezi ujao kutakuwa na mafunzo ya menejimenti na kufanya kazi kwa ubia naomba mhudhurie muongeze ujuzi,” amesema

Amesema ni vizuri kuwatumia wataalamu kwenye utekelezaji wa shughuli zao lakini wanapaswa kutokuwa wategemezi kupita kiasi hivyo watumie mafunzo hayo kujiweka sawa na kuchana na utegemezi wa kujaza zabuni na kuendesha makampuni yao.

Amesema kazi za ujenzi ziko nyingi lakini za ushindani badala ya kukaa na kulalamika kwamba hawapati kazi wayatumie mafunzo hayo kuongeza ujuzi hasa kwenye kujaza zabuni kielektroniki na kuweka bei ambayo ni halisia.

“Hakuna kazi nyingi kwamba kila mtu atapata lakini zipo za ushindani na ili uweze kushindana kwenye soko hili ni lazima uwe na ujuzi mkubwa kwenye menejimenti, kujaza zabuni na kusimamia mikataba sasa ukisikia mafunzo njoo yana faida kubwa,” amesema

Amesema Serikali imejitahidi kutangaza zabuni nyingi za miradi ya maji na ujenzi wa barabara hivyo makandarasi wa ndani wtakaobahatika kuipata wanapaswa kuitekeleza kwa ufanisi mkubwa.

“Mkifanya vizuri mnajitengenezea njia yenu nay a wengine kuaminiwa ukifanya vibaya unatuharibia nasisi kuaminiwa. Biashara hii ya ukandarasi ni nzuri tu na ya heshima kwa hiyo hakikisheni mnalinda heshima ya kazi yetu kwa kufanyakazi nzuri,” amesema
Msanifu Majengo, Neema Fuime ambaye ni Mratibu wa Mafunzo kwenye Bodi ya Usajili wa Makaandarasi (CRB), akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo, QS Joseph Tango siku ya kwanza ya ufunguzi wa mafunzo kwa makandarasi wazalendo mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma
Naibu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Injinia David Jere akisoma muhtasari wa mafunzo ya siku tatu kwa makandarasi wazalendo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma. Anayefuata ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB), Injinia Consolata Ngimbwa, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) QS Joseph.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) QS Joseph Tango akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa siku tatu kwa makandarasi wazalendo uliofanyika mkoani Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Injinia Consolata Ngimbwa na kushoto ni Mratibu wa Mafunzo wa CRB, Msanifu Majengo, Neema Fuime.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad