TAKRIBANI WATOTO 11,000 WANAZALIWA NA SIKOSELI NCHINI KWA MWAKA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 27, 2022

TAKRIBANI WATOTO 11,000 WANAZALIWA NA SIKOSELI NCHINI KWA MWAKAKatibu Mkuu wa n ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara ya Afya, Prof. Abel Makubi akizungumza jambo leo jijini Dar es Salaam katika Kongamano la kujadili mwelekeo wa ugonjwa wa sickle cell lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wadau wa Idara ya afya wakiwemo wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, wawakilishi kutoka balozi mbalimbali, Madaktari bigwa, Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Sayansi Muhimbili (MUHAS) wakiwa katika Kongamano la kujadili mwelekeo wa ugonjwa wa sickle cell nchini Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam (Picha Na Noel Rukanuga)


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Sayansi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe (wapili kutoka kushoto) akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara ya Afya, Prof. Abel Makubi katika Kongamano la kujadili mwelekeo wa ugonjwa wa sickle cell lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara ya Afya, Prof. Abel Makubi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau idara ya Afya wakiwemo wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, wawakilishi kutoka balozi mbalimbali, Madaktari bigwa katika Kongamano la kujadili mwelekeo wa ugonjwa wa sickle cell lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Tanzania ni mojawapo kati ya nchi zenye wagonjwa wengi wa siko seli duniani ambapo inakadiriwa karibu watoto 11,000 huzaliwa na ugonjwa wa sikoseli kila mwaka.

Aidha, inakadiriwa kuwa asilimia 12 hadi 20 ya watu wote nchini wana vinasaba vya ugonjwa wa siko seli kutegemea na eneo.

Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimefanya Kongamano la Kiafya kuhusiana na Ugonjwa Siko seli kwa kukutana na wadau mbalimbali wa afya na kujadiliana namna ya kuwatambua wagonjwa kuanzia wakiwa wadogo.

Watu walio katika mahusiano kuelekea kwenye ndoa {wachumba}, watarajie kuanza kupatiwa ushauri nasaha kuhusu ugonjwa wa Siko seli, Tanzania.

Serikali imeanza kufanyia marekebisho na maboresho Sera ya Afya ili kuwezesha wachumba kupata ushauri nasaha kabla ya kuingia kwenye ndoa ili kupunguza uwezekano wa kuongezeka kwa wagonjwa.

Imeelezwa kuwa baadhi ya Mataifa Barani Afrika hususani Nigeria na Ghana wameanzisha program ya namna hiyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amesema hayo amesema kongamano hilo limelenga kujadili mwelekeo mpya wa mapambano na udhibiti wa Siko seli Tanzania ambapo takribani watoto 11,000 wanazaliwa na ugonjwa ww siko seli.

Amesema, ni namba kubwa ya wagonjwa ila serikali tayari imeamua kuanzia program ya upimaji wa mapema kwa watoto {newborn screening}, na mtoto akigundulika mapema anaanzishiwa matibabu mapema.

Prof. Makubi amesema pamoja na hayo Serikali imeongeza vituo vya uchunguzi wa Siko seli hadi Hospitali za Rufaa za Kanda na baadhi ya Hospitali za Rufaa za Mikoa ikiwamo Mwananyamala, Amana, Temeke {Dar es Salaam} na Sekou Toure {Mwanza}.

"Hii inasaidia wananchi wasiende mbali kufuata huduma, tumeleta dawa za kupunguza makali ya Siko seli. Tunaendelea kuboresha zaidi hizi huduma wananchi wazipate ili tuweze kuwapunguzia mahangaiko wagonjwa hawa,” amesema

"Kama ambavyo kauli mbiu ya kongamano hili unavyosisitiza tunabadili mwelekeo jinsi ya kidhibiti Siko seli tunataka tushirikishe zaidi wananchi," amesisitiza Prof. Makubi.

Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Andrea Pembe amesema tangu mwaka 2004 chuo hicho kilianza kufanya tafiti kuhusu ugonjwa huo ambapo ilianzisha kliniki Hospitali ya Taifa Muhimbili {MNH}.

Amesema, Lengo la kwanza kabisa ikiwa ni kuhakikisha wanazuia watu kupata ugonjwa wa Siko seli na pili kusaidia wenye ugonjwa namna gani ya kutoa matibabu bora na wale wanaopewa matatizo ya muda mrefu ambayo hayafikiki waweze kuwepa huduma itakayowawezesha kuendelea na maisha yao katika ubora.

Prof Pembe amesema, Kupitia tafiti hizo imeonekana karibu asilimia 17 wana hivi vinasaba vya Siko seli na baadhi yao wanaishia katika ugonjwa kwa sababu wanakuwa na dalili mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad