HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 28, 2022

NBAA YATOA ELIMU KWA WANACHUO WA TIA

 

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) imeendelea kutoa elimu/mafunzo kwa wanafunzi wa Taasisi, Vyuo pamoja na Shule za Sekondari ikiwa na lengo la kuwajengea ufahamu kuhusu shughuli mbalimbali za Bodi na kukuza taaluma ya uhasibu.

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo Afisa wa NBAA kutoka Idara ya Elimu na Mafunzo, Ibrahim Magambo amesema si kila aliyesomea uhasibu anaweza kufanya kazi za kihasibu bali inabidi kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili kupewa cheti cha kitaaluma ili uweze kutambulika kama Mhasibu na kuweza kufanya kazi nje na ndani ya nchi.

Aliongeza kuwa wanafunzi wa Kozi nyingine ambazo hazihusiani na masomo ya Uhasibu nao wana nafasi ya kufanya mitihani ya Bodi na wataanzia masomo ya ngazi ya kwanza (foundation level) tofauti na wale waliosomea masomo ya Uhasibu  na pia waliomaliza kidato cha nne na sita na wanacheti wanaweza kufanya mitihani ya Bodi alisema Magambo

Naye Mhadhiri wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt. Modest Assenga  ameishukuru Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) kwa kuweza kufika kwenye Taasisi hiyo na kutoa elimu kwani baada ya wanafunzi hao kumaliza masoma yao itakuwa rahisi kuweza kujiunga na mitihani ya Bodi kwa kuwa watakuwa na uelewa kuhusu Bodi hiyo pamoja na CPA.

Afisa wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) kutoka Idara ya Elimu na Mafunzo, Ibrahim Magambo akitoa elimu kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya Uhasibu katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) iliyopo Dar es Salaam ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo kwa Taasisi, Vyuo pamoja na Shule za Sekondari.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA Magreth Kageya(katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na bodi hiyo wakati wa mafunzo kwa Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yalifanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt. Modest Assenga  akitoa neno kwa shukrani kwa wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) waliofika katika chuo hicho kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya Uhasibu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi ya NBAA.
Baadhi ya wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakifuatilia mada kutoka ka maofisa wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) waliofika chuoni hapo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo pamoja na namna ya kuweza kupata CPA.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad