Mbunge wa Hanang aahidi changamoto ya Maji kutatuliwa - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 27, 2022

Mbunge wa Hanang aahidi changamoto ya Maji kutatuliwa

 Na John Walter-Hanang

KUTOKANA na uhaba wa maji unayoikumba shule ya sekondari Daniel Naud iliyopo kata ya Mogitu wilayani Hanang, Mbunge wa jimbo la hilo Mhandisi Samweli Hayyuma amesema Siku chache zijazo RUWASA watasaini mkataba na waziri wizara ya Maji ili kuanza utekelezaji wa mradi utakaohudumia kata za Gehandu na Mogitu.

Akizungumza mbele ya kamati ya siasa ya wilaya ya Hanang mheshimiwa Hayyuma amesema licha ya kuwepo kwa changamoto ya maji katika shule hiyo ameitaka kamati ya shule hiyo kumalizia kuweka vigae katika sehemu iliyobaki ili shule hiyo iwe ya kisasa na inayokwenda na wakati.

Akijibu ombi la Mbunge mkuu wa wilaya ya Hanang Janeth Mayanja amesema kutokana na vifaa vya ujenzi vilivyobaki muda sio mrefu watabadili na kuchukua vigae ili wamalizie sehemu iliyobaki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad