Bodi
 ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imefanya kongamano la 12 la 
Mwaka lililowakutanisha wataalam zaidi ya 1200 ikiwa na  lengo la 
kujadili ubunifu wenye suluhisho katika utekelezaji wa Ununuzi na Ugavi 
kwa kutambua ushindani na mapinduzi ya Viwanda kwa maendeleo ya Jamii. 
Kongamano hilo lililoanza Novemba 30 hadi Desemba 03 mwaka 2021.
Akizungumza
 wakati wa kufunga Kongamono hilo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, 
Profesa Riziki Shemdoe aliyemwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, 
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu amesema 
wakurugenzi wa mamkala za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanafuata 
ushauri wa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi ili kuepusha upatikanaji wa 
hati chafu kwenye Mamlaka hizo hasa kwenye taasisi zote za Serikali.
Amesisitiza
 kuwa taaluma waliyoisomea iweniya kuleta tija na ufanisi kwenye Miradi 
ya Serikali hivyo Wataalam hao wanapaswa kuwa na weledi na pia ambao 
wanaheshimu taaluma yao.
Shemdoe
 amesema kuna waajiri ambao wanaajiri maafisa Ununuzi na Ugavi ambao 
hawajasajiliwa na Bodi kuwa wahakikishe wafanyakazi wao wawe 
wamesajiliwa na Bodi ya PSPTB ili kusaidia pale wanapokutana Wataalam 
hao kujadiliana masuala yao kwa uhuru na uwazi.
Amezitaka
 taasisi zote zilizoko chini ya Mamlaka ya Serikali ya Mitaa na 
zilizochini ya wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuhakikisha wataalamu 
wote ambao wameajiriwa lakini hawajasajiliwa na Bodi ya PSPTB 
wanasajiliwa haraka kulingana na Sheria iliyoianzisha PSPTB 
inavyoelekeza.
Katibu
 Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe  akizungumza na 
Wataalam wa Ununuzi na Ugavi pamoja na wafanyakazi wa Bodi hiyo kuhusu 
namna walivyojipanga kuwasimamia na kuisimamia taaluma hiyo ili kuwa na 
tija kwenye maendeleo ya Taifa wakati wa kufunga Kongamano la 12 
Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi  lililokuwa na kauli mbiu ya  kujadili 
ubunifu wenye suluhisho katika utekelezaji wa Ununuzi na Ugavi kwa 
kutambua ushindani na mapinduzi ya Viwanda kwa maendeleo ya Jamii. 
Kongamano hilo lililoanza Novemba 30 hadi Desemba 03 mwaka 2021.
Mkurugenzi
 Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi
 akizungumza wakati na Wataalam wa Ununuzi na Ugavi pamoja na 
kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Profesa 
Riziki Shemdoe aliyemwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za 
Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu kwa ajili ya kufunga 
Kongamano la 12 la mwaka la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
Baadhi
 ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi  wakifuatilia mada kwenye Kongamamo la 
12 la wataalam hao lililoanza Novemba 30 hadi Desemba 03 mwaka 2021 
likiwa na kauli mbiu ya  kujadili ubunifu wenye suluhisho katika 
utekelezaji wa Ununuzi na Ugavi kwa kutambua ushindani na mapinduzi ya 
Viwanda kwa maendeleo ya Jamii.  
Meneja
 Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee akizungumza jambo 
kwenye kongamano la 12 la mwaka la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi 
Katibu
 Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe akiwa kwenye picha 
ya pamoja na makundi mbalimbali mara baada ya kufunga Kongamano la 12 la
 Mwaka la  Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi  lililofanyika jijini Arusha.
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment