HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 4, 2021

Wakufunzi 46 ARU kusomeshwa Shahada za Uzamivu

 Msafara ukiingia kwenye viwanja vya mahafali hayo ya 15 ya ARU yaliyofanyika jana chuoni hapo.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Jaji Mkuu Othman Chande akimtunuku Shahada ya Uzamivu (PhD), mmoja wa wahitimu kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho yaliyofanyika Jumamosi chuoni hapo.*Chande asimikwa rasmi kuwa Mkuu wa ARU

Na Mwandishi Wetu
JAJI Mkuu mstaafu Othman Chande amesimikwa rasmi kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU)

Jaji amesimikwa leo Desemba 4, 2021na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Salome Sijaona, wakati wa mahafali ya 15 ya chuo hicho jijini Dar es Salaam

Akizungumza kwenye mahafali hayo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa amesema, Chuo hicho kimeshiriki kufanya tafiti 41 zisizo za Uzamivu na tafiti 62 za Uzamivu ambazo zinalenga kutoa suluhisho kwenye masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo mazingira, ardhi, makazi ya watu na ujenzi wa miundombinu.

Katika mahafali hayo wahitimu 982 walitunukiwa shahada mbalimbali ambapo 929 walipata shahada za awali, Shahada za Uzamili 45, shahada za Uzamivu 4 na Diploma 4.

Amesema chuo kimepata mradi unaolenga kufanya tafiti zitakazotatua changamoto mbalimbali ambapo kupitia mradi huo wakufunzi 54 wa ARU watasomeshwa kwa nagzi ya Shahada za Uzamili na 46 Shahada za Uzamivu .

Profesa Liwa amesema mwaka huu chuo kimepata miradi mikubwa mitatu mmmoja kwa ufadhili wa serikali ya Ubelgiji kupitia shirika la VLIR (Flemish Inter-University Council), Chuo kimepata mradi unaolenga kufanya tafiti zitakazotatua changamoto zinazolikumba jiji la Dar es Salaam ambazo zimechangiwa kwa kiasi kikubwa na uendelezaji holela wa Jiji.

Amesema mradi huo una miradi midogo saba ya utafiti na kupitia mradi huo, kitaanzishwa kituo cha umahiri cha mafunzo ya uendelevu wa miji (The African Centre for Sustainable Cities Studies).

Profesa Liwa amesema mradi huo utatoa ufadhili kwa kusomesha wakufunzi wa ARU wapatao (54) kwa Shahada za Uzamili na 46 kwa Shahada za Uzamivu kwa muda wa miaka kumi.

Ameutaja mradi mwingine kuwa ni wa ushiriki wa watu wenye umri mdogo katika masuala ya mabadiliko ya Tabia Nchi Tanzania (Young People’s Climate Change Engagement in Tanzania (Y-ENGAGE))”.

“Mradi huu unalenga kuongeza uelewa na ushiriki wa vijana wa Tanzania katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na unafadhiliwa na Serikali ya Denmark kupitia shirika lake la DANIDA,” alisema.

Ameutaja mradi mwingine kuwa ni wa uanzishwaji wa maaabara za uzalishaji viwandani (Industrial Automation laboratories).

Amesema chuo kwa ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya kimeanzisha maabara hiyo ambayo itatumika kufundishia wanafunzi mifumo mbalimbali ya kisasa zaidi ya uzalishaji katika viwanda mbalimbali.

“Kutokana na kuwa vifaa vilivyofungwa kwenye maabara hii ni vya kisasa, wahitimu katika fani ya mifumo ya kompyuta watahitimu wakiwa tayari wana ujuzi wa kuwawezesha kufanya kazi moja kwa moja bila kupata mafunzo makubwa. Hii itaongeza na kurahisisha ajira kwa wanafunzi wetu,” alisema.

Amesema chuo kimesanifu, kusimamia ujenzi na kutoa ushauri katika miradi mbalimbali ya Serikali, taasisi zake, mashirika ya umma na kampuni binafsi.

Mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, Balozi Salome Sijaona ameippshukuru na kuipongeza Menejimenti ya Chuo chini ya Uongozi wa Profesa Evaristo Liwa kwa kupanga na kusimamia vyema utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo za Chuo na hivyo kuwa na matokeo mazuri na ya haraka ya mipango ya maendeleo.

“Ni matumaini yangu kuwa kasi hiyo itaendelea ikiwa pia ni matazamio ya Serikali yetu kuwa malengo ya uanzishwaji wa Chuo hiki yanafanikiwa na kutekelezwa katika ubora uliokusudiwa,” amesema Profesa Mahalu.

“Ninaupongeza Uongozi wa Chuo kwani licha ya changamoto ya mlipuko wa ugonjwa wa uviko-19 bado Chuo Kikuu Ardhi kwa kuzingatia miongozo ya kujikinga na ugonjwa huu kimeendelea kujizatiti kwa kuendelea kutekeleza majukumu ya uanzishwaji wake ikiwemo ya kimasomo, Utafiti na Ushahuri wa Kitaalam kwa Taifa.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Balozi Salome Sijaona akimvisha kofia Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande kama ishara ya kumsimika rasmi kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu hicho wakati wa mahafali ya 15 ya chuo hicho yaliyofanyika Jumamosi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa na kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho taaluma.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa (kushoto) akizungumza na Mkuu wa chuo hicho, Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande, wakati wa mahafali ya 15 ya chuo hicho yaliyofanyika siku ya Jumamosi chuoni hapo. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Balozi Salome Sijaona.

Sehemu ya wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), wakiwa kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho yaliyofanyika siku ya Jumamosi kwenye viwanja vya chuo hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa chuo hicho Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande na Mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, Salome Sijaona.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad