PSSSF YATWAA TUZO YA UMAHIRI UWASILISHAJI BORA WA TAARIFA ZA MAHESABU 2020 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 4, 2021

PSSSF YATWAA TUZO YA UMAHIRI UWASILISHAJI BORA WA TAARIFA ZA MAHESABU 2020

 

 

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetwaa Tuzo ya Umahiri katika Uwasilishaji wa Taarifa za mahesabu kwa mwaka 2020.
Akizungumza baada ya kupokea Tuzo hiyo katika hafla ya kufunga mafunzo pamoja na utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2020 (Best Presented Financial Statements for the Year 2020 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam Desemba 4, 2021, Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi alisema Ushindi huo ni ishara ya kwamba PSSSF inaandaa mahesabu kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kimataifa lakini pia inaashiria uwepo wa weledi wa tasnia husika kwa upande wa watumishi.

“Sambamba na hayo niliyoyasema pia inaashiria uwepo wa usimamizi makini wa fedha za wanchama na hii inatupatia heshima kama taasisi.” Alisema Mkurugenzi huyo wa Fedha PSSSF.

Aliwahakikishia Wanachama dhamira ya PSSSF kuhakikisha usalama wa michango yao unazingatiwa kwa kiwango cha juu wakati wote, ikiwa ni pamoja na kuwepo uwazi kwenye usimamizi na utunzaji wa rasilimali za Mfuko.
“Ushindi huu pia unaashiria uwepo wa kesho ya wanachama wetu kama kaulimbiu yetu inavyosema Leo. Kesho. Pamoja.” Alihitimiaha Bi. Beatrice Musa-Lupi
Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi (kulia) akipokea tuzo hiyo kutoka kwa mgeni rasmi, Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Leonard Mkude.
Washindi wa Kwanza wa tuzo zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu
Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi (kulia) na Bi. Grace Kabyemela, Mhasibu Mkuu wa PSSSF wakionyesha tuzo hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad