T-MARC TANZANIA YATOA MSAADA WA DAWA ZA UZAZI WA MPANGO PAMOJA NA TAULO ZA KIKE MBEYA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 4, 2021

T-MARC TANZANIA YATOA MSAADA WA DAWA ZA UZAZI WA MPANGO PAMOJA NA TAULO ZA KIKE MBEYA

 

Viongozi na wawakilishi wa T-MARC Tanzania Alpha Joseph Pamoja na Lilian Mallya wakitoa msaada wa dawa za uzazi wa mpango za FlexP na Revoke kwa Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya Dr. Osmunda Mwanyika (katikati) akiwa na Muuguzi mkuu wa mkoa  Elesia George pamoja na  Mratibu wa huduma za afya ya uzazi na watoto Magdalena Manjano. Taasisi hii pia inatoa elimu kwa maduka ya dawa baridi nchini juu ya utumiaji sahihi wa dawa hizi za afya  za uzazi wa mpango  na inategemea kufikia walengwa (akina mama na mabinti) nchi nzima.
Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mbeya Dr. Osmunda Mwanyika akipokea msaada wa dawa za uzazi wa mpango kutoka Taasisi ya T-MARC Tanzania kupitia mabalozi wake Dr Isaac Maro na DR Romana kama sehemu ya huduma za kijamii. “Dawa hizi za uzazi wa mpango zitaenda kusaidia wakina mama na mabinti kupangilia afya yao ya uzazi kwa kutumia dawa bora na salama tulizokabidhiwa na taasisi ya T-MARC Tanzania”  Dr. Osmunda Mwanyika .
Taasisi ya T-MARC Tanzania imetembelea na kutoa msaada wa  taulo za kike kwa wasichana wa shule ya sekondari loleza jijini Mbeya, huku wakisindikizwa na mabalozi wa taulo hizi za Flowless pads, Monalisa, Dr Romana na Dr Isaac Maro. Pamoja na msaada wa taulo hizo mabalozi hao walipata muda wa kuzungumza na mabinti katika shule hii ya Loleza kuhusu umuhimu wa kuzingatia masomo ili kufikia ndoto walizonazo.
Baadhi ya wawakilishi wa wanafunzi kutoka shule ya Loleza High School iliyopo Mbeya Pamoja na Mwalimu Mkuu wakipokea msaada wa taulo za kike kutoka kwa Balozi wa taulo hizi  za Flowless Pads,  Dr Romana zinazosambazwa na taasisi ya T-MARC Tanzania, ikiwa ni moja ya sehemu ya huduma za kijamii. Pamoja na utoaji wa msaada huu wa wa taulo hizi, wanafunzi hawa walipokea elimu ya hedhi salama na kusisitiziwa kusimamia masomo ili kufikia malengo yao maishani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad