Benki ya CRDB, WorldRemit kurahisisha huduma ya Utumaji na upokeaji Pesa Kimataifa - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 7, 2021

Benki ya CRDB, WorldRemit kurahisisha huduma ya Utumaji na upokeaji Pesa Kimataifa

Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wa kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya itakayowawezesha Watanzania kutoka mataifa zaidi ya 50 kote duniani kutuma na kutoa pesa kupitia Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika linalotoa huduma ya kutuma pesa kidijitali la 'WorldRemit', iliyofanyika leo kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkaazi na Msimamizi Mkuu kwa ukanda wa Afrika Mashariki wa WorldRemit,  Cynthia Ponera na kushoto ni Meneja Mwanadamizi wa Huduma Mbadala Benki ya CRDB, Mangire Kibanda. 
 
======   ======    ======

Benki ya CRDB kwa kushirikiana na shirika linalotoa huduma ya kutuma pesa kidijitali WorldRemit, leo zimetangaza ushirikiano unaowarahisishia Watanzania mchakato wa kutuma pesa kidigitali kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Huduma hii mpya itawawezesha raia Watanzania kutoka mataifa zaidi ya 50 kote duniani kutuma na kupokea pesa kupitia mtandao wa zaidi ya matawi 260 ya Benki ya CRDB.

Akizunguma katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wa kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema kuwa Benki ya CRDB imefurahishwa na ushirikiano wao na WorldRemit, Huku kukiwa na raia wengi wanaofanya kazi nchi mbalimbali,  hivyo wamejitolea kufanya utumaji pesa kuwa rahisi na salama. 

"Huduma hii ya kutuma pesa inafanyika haraka na kwa gharama nafuu sana. Kwa sasa, wateja wetu wanaweza kupata huduma hii ya kutuma na kupokea pesa katika matawi yetu yote 260 yaliyoenea nchi nzima na hivi karibuni tunategemea kuongeza wigo kwa kutumia mawakala wa Benki ambao ni zaidi ya 20,000 nchi nzima”.
Kupitia ushirikiano huu, WorldRemit inaendelea kutanua wigo wake katika soko ulimwenguni na katika juhudi za kufanya huduma za kutuma pesa kimataifa kupatikana kirahisi na kwa bei nafuu. Hatua hii itasaida kuwezesha malipo kutoka kwa Watanzania wanaoishi ugenini, wanaosaidia kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini. 

Mkataba kati ya WorldRemit na Benki ya CRDB ulizinduliwa Novemba 16, 2021, na utawezesha shughuli ya utumaji pesa kimataifa, Hii inamaanisha Watanzania wanaoishi nchi za nje hawatahitajika tena kuwa na hofu iwapo fedha wanazotumia familia na marafiki zao zitawafikia kwa wakati sahihi hasa kuelekea katika msimu wa Sikukuu ya Krismasi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi na Msimamizi Mkuu kwa ukanda wa Afrika Mashariki wa WorldRemit, Cynthia Ponera, aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuingia mkataba huo kama ushirikiano muhimu unaorahisisha mchakato wa utoaji huduma bora ya utumaji na upokeaji wa pesa kimtandao. Alisisitiza kuwa “Ujumushaji wa kifedha ndicho kiini cha ushirikiano huo. Mtandao mpana wa matawi ya Benki ya CRDB utafikia Watanzania kote nchini na kuwawezesha kutoa kirahisi pesa walizotumiwa kimataifa kupitia WorldRemit, pamoja na kuwezesha raia wanaoishi katika mataifa zaidi ya 50 kupata huduma hizi.”

WorldRemit inathamini usalama wa pesa za wateja wake na hutumia teknolojia ya hali ya juu kuhakikisha usalama wa pesa hizo ili kuepukana na udanganyifu na wizi wa kimtandao. Jifahamishe zaidi: www.worldremit.com
Meneja Mwanadamizi wa Huduma Mbadala Benki ya CRDB, Mangire Kibanda akifafanua jambo katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya itakayowawezesha Watanzania kutoka mataifa zaidi ya 50 kote duniani kutuma pesa kupitia Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika linalotoa huduma ya kutuma pesa kidijitali la 'WorldRemit', iliyofanyika leo kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad