Mamlaka
ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeadhimisha Siku ya Kimataifa ya
Usafiri wa Anga Duniani yaani International Civil Aviation Day (ICAD)
iliyofanyika leo Desemba 07, 2021 ikiwa na kauli mbiu isemayo “Ubunifu
Endelevu kwa Maendeleo ya Usafiri wa Anga Duniani”
Maadhimisho
hayo yamefanyika leo Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania(TCAA) yaliyopo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza
na watumishi, Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka hiyo, Teophory Mbilinyi
aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Hamza Johari amesema
desturi ya sekta hii ya Usafiri wa Anga duniani ifikapo Desemba 07 kila
mwaka huwa wanaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga hivyo kwa
mwaka 2021 Mamlaka imetekeleza mambo mbalimbali kama sehemu ya
maadhimisho ya ICAD.
“Kuanzia
Desemba 01 mpaka 03 TCAA kwa kutumia mameneja wa vituo 14 walienda
redioni na kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga, fursa
zinazopatikana pamoja na kukinadi chuo chetu cha usafiri wa anga yaani
CATC. Hivyo mameneja hao wameipeperusha vyema bendera ya TCAA kwa
kueleza kwa kina masuala ya msingi ya Mamlaka hii” alisema Mbilinyi
Mbilinyi
amesema Desemba 05 mwaka 2021 TCAA iliandaa mbio fupi zilizokuwa na
jina “Fun Run” iliyohusisha watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Shirika la
Ndege la Tanzania(ATCL), Shirika la ndege la Precision pamoja na wadau
mbalimbali wa Usafiri wa Anga hapa nchini.
Pia
alitumia nafasi hiyo kuwapongeza washiriki wote wa mbio hizo na
kuwakumbusha kuwa kufanya mazoezi ni jambo la muhimu sana kwa sasa hasa
ukizingatia yanasaidia katika kujikinga na magonjwa mbalimbali
yasiyoambukiza.
Pia
amesema Desemba 06 Mamlaka hiyo ilitoa msaada wa vitanda vya double
decker 26 vitakavyohudumia wanafunzi 52 katika Shule ya Sekondari Azani
na kusisitiza kuwa TCAA itaendelea kusaidia jamii kwenye masuala
mbalimbali ya kijamii ikiwa pia ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za
Serikali katika elimu na Nyanja nyingine za kijamii.
“Ili
kuendelea kujikinga na UVIKO-19 TCAA tumeleta wataalamu wa afya kwa
ajili ya kutoa chanjo ya UVIKO-19 kwa watumishi na nimearifiwa kuwa
baadhi ya watumishi wamepatiwa chanjo hiyo hivyo nawaomba wale ambao
hawajachanjwa kuchanja ili kuwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan
aliyeonesha mfano kwa kuchanjwa hadharani”. Alisema Mbilinyi
Amewasisitiza
Watumishi kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa
na Mhe. Rais Samia kwa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kuweza
kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri wa anga hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Teophory
Mbilinyi(kulia) akipanda mti pamoja na Mkaguzi Mkuu Kiongozi wa Usalama
wa Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Majaliwa Buruhani(kushoto) wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani ikiwa na kauli mbiu isemayo
“Ubunifu Endelevu kwa Maendeleo ya Usafiri wa Anga Duniani ” yaliyofanyika
leo Desemba 07, 2021 Makao makuu ya Mamlaka hiyo Ukonga-Banana jijini Dar es
Salaam leo. Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka hiyo, Teophory Mbilinyi
aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania
(TCAA) Hamza Johari.
Mkurugenzi
wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Teophory
Mbilinyi akiwa kwenye picha ya pamoja Menejimenti ya Wafanyakazi wa
Mamlaka hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa
Anga Duniani yaliyofanyika leo Desemba 07, 2021 Makao makuu ya Mamlaka
hiyo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam leo.
Maandamano
yakiendelea wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa
Anga Duniani yaliyofanyika leo Desemba 07, 2021 Makao makuu ya Mamlaka
hiyo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Teophory
Mbilinyi akipokea maadamano ya Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani
yaliyofanyika leo Desemba 07, 2021 Makao makuu ya Mamlaka hiyo Banana
jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment