Mkoa
 wa Iringa wenye kumiliki asilimia 40 ya misitu ya kupandwa nchini 
Tanzania na ni moja ya sehemu zenye aridhi bora sana kwa ajili ya kilimo
 cha miti duniani. Ili kutumia fursa hii mkoa wa Iringa umeandaa 
kongamano kubwa la uwekezaji katika sekta ya misitu.
Akifungua
 kongamano hilo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa pongezi kubwa kwa 
mkoa na pia kueleza msimamo wa Serikali ya awamu ya sita katika 
kuchochea uwekezaji nchini. Pia Waziri Mkuu aliagiza makampuni yenye 
kuchakata mazao ya misitu kuhakikisha yanatengeneza bidhaa bora na 
kutosafirisha bidhaa ghafi.
Waziri
 Mkuu aliuelezea mkoa wa Iringa kama eneo bora la uwekezaji likiwa na 
muunganiko mzuri wa barabara na muda mfupi ujao kwa ndege baada ya 
kukamilika kwa uwanja wa ndege wa Iringa.
Mkuu
 wa Mkoa wa Iringa Queen Sendega alisema mkoa wake uko tayari kusaidia 
wafanya biashara kufanya biashara kwa urahisi kwa kuweka mazingira 
wezeshi.
Kabla
 ya kufungua kongamano hilo alizindua chapa ya Iringa woodland ikiwa ni 
lengo la mkoa wa Iringa kuchagiza ukuaji wa utengenezaji wa bidhaa za 
mbao, kuutangaza mkoa na pia utalii. 
Akizungumza
 wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Gofin Ventures Imani Kajula 
ambao ni waandaaji wa kongamano hilo na mkakati wa kujenga chapa ya 
Iringa woodland alisema " hii ni fursa pana kwa mkoa wa Iringa kufaidika
 na sekta ya utalii, misitu na pia kuutangaza mkoa wa Iringa ndani na 
nje ya Tanzania" pia kutoa ajira kwa vijana ambao watatumia chapa ya 
Iringa woodland kutengeneza bidhaa mbali mbali

No comments:
Post a Comment