HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 14, 2021

MSHINDI WA TUZO ZA LIPFF AWASILI NCHINI, BASATA WAMPONGEZA


Mwandishi, muigizaji na mwanamitindo, Regina Kihwele 'Gynah' akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufika katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

BARAZA la Sanaa Tanzania (BASATA) limempongeza Mwandishi, muigizaji na mwanamitindo, Regina Kihwele 'Gynah' aliyeibuka mshindi wa muigizaji bora kike kwenye tuzo za Lake International Pan African Film Festival (LIPFF) zilizofanyika usiku wa Novemba 6, 2021 nchini Kenya.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa BASATA, Gaima Baraka amesema kuwa wameanza kuchukua jukumu la kuendeleza vipaji vya wasani hapa nchini.

Amesema kuwa Sanaa ya Tanzania inatangazwa ndani na nje ya nchi ili dunia ijue kuwa Tanzania inautamaduni na ndio kiini cha kuendeleza taifa letu, Sanaa ni Biashara kwahiyo kila msanii anayefanya sanaa anakwenda kufanya sanaa kibiashara ili sanaa imletee manufaa.

Ametoa wito kwa wasanii kuwa na weredi katika sanaa na kufanya sanaa kwa kumaanisha pia wafanye sanaa kwa uhalisia wake na kufanya sanaa bila kuharibu sanaa ya Tanzania.

Baraka mesema kuwa watanzania na wasanii kwa ujumla waepuke sanaa inayoharibu taswira ya sanaa ya Tanzania na tutangaze nchi yetu kwa mlengo wenye kuleta manuufaa ya nchi na kuwa mabalozi wa sanaa na utamaduni wa sanaa ya kitanzania popote pale.

Basata inahakikisha inaendeleza sanaa na utamaduni wa Mtanzania.

Mwandishi, muigizaji na mwanamitindo, Regina Kihwele 'Gynah akizungumza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere alisema kuwa anaomba jamii imuunge mkono katika kazi zake za kisanaa.

Amewaomba pia watanzania kuuunga mkono sanaa ya Tanzania ili kuweza kuendeleza Taifa kwa manufaa ya watanzania wote licha ya hayo Gynah amewaasa wanajamii wanaotaka kufikia hatua kama yake wapende wanachokifanya na kujituma kwa bidii wanapopewa nafasi ya kufanya kazi wafanye kweli kwa kumaanisha.

Kwa upande wa Mama Mzazi wa Gynah, amesema kuwa mambo mazuri zaidi yanakuja katika  kuendeleza sanaa hapa nchini kutokana na uwezo wake kwani ameshafikia kushinda tuzo ya mwigizaji bora wa Lake International Pan African Film Festival (LIPFF).

Licha ya hayo amewaasa wazazi kuwaunga mkono watoto wanapowaona watoto wakiwa na taranta kwenye fani yeyote ambayo anaweza kufanya.

"Wazazi tuwe mstari wa mbele kukuza vipaji vya watoto wetu kwa sababu mambo yote yanaanzia nyumbani na baadae anaendelea juu zaidi." Alisema.

Gynah aliwabwaga waigizaji wengine kutoka, Afrika Kusini, Cameroon, Morocco na Uganda katika shindano la (LIPFF).
Wanafamilia ya Mwandishi, muigizaji na mwanamitindo, Regina Kihwele 'Gynah' akimpokea mwanae mara baada ya kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea nchini Nairobi ambako tuzo za Lake International Pan African Film Festival (LIPFF) zilifanyika.
Mwandishi, muigizaji na mwanamitindo, Regina Kihwele 'Gynah' akiwa katika lango la uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea nchini Nairobi ambako tuzo za Lake International Pan African Film Festival (LIPFF) zilifanyika.

Mwandishi, muigizaji na mwanamitindo, Regina Kihwele 'Gynah' akionesha tuzo ya mwigizaji bora wa kike katika shindano la tuzo za Lake International Pan African Film Festival (LIPFF) zilizofanyika Nairobi Nchini Kenya.
Mwandishi, muigizaji na mwanamitindo, Regina Kihwele 'Gynah', Wawakilishi wa Baraza la Sanaa Tanzani na wanafamilia wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad