WAWATA DEKANIA YA MT. GASPAR WAZIDUA MIAKA 50 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 14, 2021

WAWATA DEKANIA YA MT. GASPAR WAZIDUA MIAKA 50

Wenyeviti WAWATA dekania ya Mtakatifu Gaspar akiwa na mishumaa kwaajili ya kuwashwa na Padre kwaajili ya uzinduzi wa Miaka 50 ya WAWATA katika Dekania ya Mtakatifu Gaspar jimbo kuu la Dar es Salaam, uzinduzi huo umefanyika katika kiwanja vya Dekania ya Gaspar kilichopo Mabwepande Novemba 13,2021.

WANAWAKE wakatoliki Tanzania (WAWATA) wa Dekania ya Mtakatifu Gaspar De Bufalo wamezindua jubilei ya Miaka 50 ya iliyofanyika Mabwepande jijini Dar Es Salaam, Novemba 13, 2021.

Uzinduzi huo uliambatana na Semina ya Afya ya Akili kutoka utoto hadi kuzeeka iliyowasilishwa na Daktari Esta Kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili. 

Shamra shamra za zilisindikizwa na kwaya ya WAWATA dekania ya Gaspari huku Mashangwera kutoka katika kila Parokia zinazounda Dekania ya Mt. Gaspar wakatao timiza miaka 50 hapo mwakani kuanzishwa hapa nchini (1972-2022).

Mashangwera ni wale Wanawake wa Katoriki Tanzania waliozaliwa Mwaka mmoja na Utume wa WAWATA, Utume wa huo uliingia hapa nchini Mwaka 1972.

Makamu mwenyekiti wa parokia ya thoma mtume Goba, bi. prisca Mkinga akiwa na mshumaa mara baada ya kuwashwa na Padre kwaajili ya uzinduzi wa Miaka 50 ya WAWATA katika Dekania ya Mtakatifu Gaspar jimbo kuu la Dar es Salaam, uzinduzi huo umefanyika katika kiwanja vya Dekania ya Gaspar kilichopo Mabwepande.

Padre wa Parokia ya Mabwepande akiwamwagia maji ya Baraka Mashangwera wa Dekania ya Mtakatifu Gaspar jimbo kuu la Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Miaka 50 ya WAWATA jimbo kuu la Dar es Salaam.

Mashangwera wakiwa na Nyuso za furaha mara baada ya kuzinduliwa kwa miaka 50 ya WAWATA jimbo kuu la Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya wenyeviti wa parokia WAWATA na mapadre.
Kwaya ya Dekania ya Mtakatifu Gaspar wakimsikiliza Msheheleshaji katika wa uzinduzi wa Miaka 50 ya WAWATA katika dekania hiyo.
Wawata wakiwa na nyuso za Taasamu wakati wa uzinduzi wa miaka 50 ya WAWATA.


Mashangwera wakifyatua maparashuti wakati wa uzinduzi wa miaka 50 ya WAWATA katika viwanja vya Mabwepande Novemba 13,2021.

Makamu mwenyekiti wa parokia ya thoma mtume bi. prisca Mkinga akiwapekelea WAWATA wa parokia yake Mshumaa uliowashwa kwaajili ya uzinduzi wa miaka 50 ya WAWATA, hafla ya uzinduzi imefanyika Mabwepande jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa WAWATA Dekania ya Makatifu Gaspar wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasha mishumaa kuashiria uzinduzi wa miaka 50.
Wanakwaya wakiimba katika uzinduzi wa miaka 50 ya WAWATA hapa nchini.WAWATA parokia ya thoma mtume Goba wakiwa katika vyombo vya usafiri kuelekea Nyumbani mara baada ya kuzindua miaka 50 ya WAWATA katika kiwanja cha Dekania kilichopo Mabwepande jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad