Ingawa matumizi ya pesa taslimu bado ni makubwa nchini, maendeleo ya malipo kufanyika kidijitali yanaridhisha huku Benki ya NMB ikichangia mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa.
Mwishoni
 mwa juma lililopita mchango wa NMB kwenye harakati za kuifanya Tanzania
 iwe nchi ya uchumi wa kidijitali ulitambuliwa kimataifa na kampuni ya 
Mastercard International.
Kampuni
 hiyo kigogo wa teknolojia bunifu duniani iliitunuku NMB tuzo maalum 
kutambua uwekezaji inayoufanya kusaidia kupunguza matumizi na kutegemea 
sana pesa taslimu.
NMB ilipewa tuzo hiyo baada ya kuibuka benki kiongozi wa kukuza na kuhamasisha matumizi ya kadi za malipo za Mastercard nchini.
Tuzo
 hiyo pia inadhibitisha kujitolea kwa NMB kuziimarisha huduma jumuishi 
za kifedha na kuwa mstari wa mbele kuweka misingi madhubuti ya mifumo ya
 malipo ya kidijitali.
Nishani
 iliyopewa NMB na Mastercard Ijumaa jijini Dar es Salaam ni baada ya 
kufanikiwa kukuza matumizi ya malipo ya kadi kwa kasi kubwa sana.
Katika
 kufanya hilo, NMB ilivunja rekodi yake yenyewe ya kiasi cha pesa 
kilichotumika katika vituo vya mauzo kwa kutumia kadi huku thamani ya 
matumizi hayo ikiongezeka kwa asilimia 30 ndani ya mwaka mmoja.
Kwa
 mujibu wa Mastercard, ni NMB pekee nchini na katika ukanda huu ambayo 
imefanikiwa kuongeza matumizi ya kadi za malipo kwa zaidi ya asilimia 
100 katika kipindi cha miezi 12.
Afisa
 Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa benki hiyo, Bw. Filbert Mponzi, 
alisema mafanikio yaliyoifanya NMB kuibuka kidedea yalipatikana kati ya 
Juni 2020 na Juni 2021.
“Tuzo
 hii ni kielelezo tosha kabisa cha ukubwa wa Benki ya NMB nchini 
inayochagizwa na upana wa mtandao wake wa matawi 226 na wateja zaidi ya 
milioni nne,” kiongozi huyo alinena kabla ya kupokea tuzo ya Mastercard.
“Hii
 ni tuzo ya kwanza ya namna hii kuwahi kutolewa kwa benki hapa nchini 
Tanzania. Asanteni sana wenzetu wa Mastercard na pia shukrani nyingi kwa
 wateja wa NMB waliotufanya kutambuliwa na Mastercard,” Bw. Mponzi 
alisema.
Sababu
 zilizopelea ushindi huu wa kidijitali wa NMB ni mbili. Kwanza ni idadi 
kubwa zaidi ya wateja wanaotumia kadi kuliko benki yoyote nchini. Zaidi 
ya wateja wa NMB milioni tatu wanatumia kadi za Mastercard kwa ajili ya 
huduma mbalimbali za kifedha idadi ambayo haijafikiwa na benki nyingine 
zote nchini.
Bw.
 Mponzi alisema sababu ya pili ni kiasi kikubwa cha pesa kilichotumika 
katika vituo vya malipo kwa kutumia kadi za NMB MasterCard ambacho 
kiliongezeka kwa asilimia 104 ndani ya mwaka mmoja.
“Mbali
 na sababu hizi, Benki ya NMB imekuwa kinara katika kuhamasisha matumizi
 ya kadi sio tu kwa ajili ya kutolea pesa katika ATM bali na katika 
matumizi mengine mengi kama kufanya malipo katika sehemu za migahawa, 
supermarket, vituo vya mafuta na katika sehemu za starehe na hata 
kuagiza bidhaa mbalimbali kupitia mitandao.”
Bw
 Mponzi alisema kutambuliwa mchango wa NMB kwenye mafanikio ya nchi 
kidijitali ni sifa nyingine ya taasisi hiyo kutokuwa na mpinzani sokoni 
na tuzo ya Mastercard ni moja ya nyingi za ubora ilizotunukiwa mwaka 
huu.
Aidha,
 alisema NMB pia ni mahili katika maeneo mengine kama kuongoza kupata 
faida pamoja na kuwa na kiasi kikubwa cha amana na rasilimali fedha.
Ili
 kuendeleza uongozi huo, Bw Mponzi aliweka wazi mikakati ya NMB kwa 
ajili ya hilo akisisitiza kuepukana na ubaili kwenye uwekezaji na 
umuhimu wa ubunifu.
“Benki
 ya NMB itaendelea kubuni suluhisho mbalimbali zenye lengo la kuboresha 
matumizi ya kadi na kwa kutumia teknolojia mbalimbali,” alibainisha
“Ni
 imani yetu kuwa idadi ya watumiaji wa kadi itazidi kuongezeka na hata 
miamala kupitia kadi itaongezeka zaidi,” aliongeza na kuisifia 
Mastercard kwa ubobezi wake katika teknolojia ya kadi za malipo.
Mwaka
 2014, NMB na Mastercard walikubaliana kushirikiana kutumia malipo ya 
kielektroniki kuchochea uchumi wa kidijitali na kuwa sehemu ya ajenda ya
 taifa ya kufanikisha huduma jumuishi za kifedha.
Meneja
 wa MasterCard Afrika Mashariki, Bw Shehryar Ali, alisema tuzo ya NMB ni
 zaidi ya kuwezesha matumizi ya kadi kwani benki hiyo imefanya mengi 
kusaidia kupunguza matumizi ye pesa taslimu na kuendeleza huduma za 
kifedha nchini.
“Matumizi
 ya pesa taslimu ambayo yanafikia hadi asilimia 90 ya miamala yote 
inayofanyika Tanzania yanaughalimu uchumi wa nchi asilimia mbili za pato
 la taifa kwa sababu lazima pesa hizo zichapishwe, zihifadhiwe, 
zisafirishwe na zilindwe,” Bw Ali alifafanua.
Afisa 
 Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi 
(wapili kulia) akionyesha Tuzo ya MasterCard iliyokabidhiwa kwa Benki ya
 NMB  na  Mkurugenzi Mkazi wa Afrika Mashariki wa MasterCard, Shehrya 
Ali wakati wa hafla iliyofanyika Dar es Salaam.Kulia ni  Mkuu wa 
Biashara ya Kadi wa Benki ya NMB, Philbert Casmir na kushoto ni Mkuu wa 
Biashara wa Master Card, Victor Ndlovu.

No comments:
Post a Comment