Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,ametembelea kuona maendeleo ya
Ujenzi wa Mradi wa Bwawa Kubwa la Maji litakalogharimu Shilingi Milioni
900 huko Mjembe, Kwamduma linalojengwa na Wakala wa Maji
Vijijini-RUWASA.
Akizungumzia ujenzi huo ,alieleza bwawa hilo ,litakapokamilika litapeleka maji kwa Vitongojj vyote kwa kijiji cha Kwamduma.
Ridhiwani alisema maji safi ni muhimu kwa afya za binadamu hivyo watarajie wakazi hao kuondokana na kero ya maji.
Ridhiwani Pia ameongea na wananchi na kuwaasa kujikinga kupambana na gonjwa la Korona na kwenda kuchanja.
Aliwaondoa hofu na kuwataka wakachanjwe kwa hiari zao na kuwaambia Chanjo hiyo haina madhara .
#AsanteSerikali #KaziInaendelea
No comments:
Post a Comment