HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 5, 2021

MAKAMU WA RAIS MSIBANI KWA WAZIRI KWANDIKWA

 

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akisaini kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias John Kwandikwa , Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani. Pembeni ni Mke wa Makamu wa Rais Bi. Mbonimpawe Mpango. Agosti 4,2021.

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akimfariji mke wa marehemu Elias John Kwandikwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Bi. Marceline Kwandikwa pamoja na mtoto wa Marehemu (Kushoto) Jackline Kwandikwa Wakati alipofika kuwapa faraja familia hiyo  nyumbani kwa marehemu Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani. Agosti 4,2021.

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Mwansansu wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Elias Kwandikwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani. Agosti 4, 2021.


Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akizungumza na waombolezaji waliojitokeza nyumbani kwa marehemu Elias Kwandikwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani. Agosti 4, 2021.

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman Msuya mara alipowasili kuwapa pole kufuatia kifo cha kaka wa Mkurugenzi huyo Bw. Bisward Msuya kilichotokea Agosti 3, 2021. 

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  Akimfariji Bi. Lisa Msuya ambaye ni mke wa marehemu Bisward Msuya mara alipofika kuitembelea familia hiyo eneo la Tangi Bovu jijini Dar es salaam. Agosti 4, 2021.



Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akizungumza na waombolezaji waliojitokeza nyumbani kwa marehemu Bisward Msuya ambaye ni kaka wa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman Msuya. Agosti 4, 2021.

 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad