Rais Mwinyi apokea vifaa vya ujenzi kutoka NMB - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 13, 2021

Rais Mwinyi apokea vifaa vya ujenzi kutoka NMB

 

Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya kuezekea kituo cha afya Jang’ombe kilichopo visiwani Zanazibar. Msaada huo ni mabati 255, mbao 220 na kilo 100 za misumari vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 13.

Msaada huo umepokelewa na kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi wakati wa ziara yake kituoni hapo.

Rais Mwinyi, aliipongeza benki ya NMB kwa kutoa msaada huo na juhudi zake katika kuendelea kuzisaidia jamii zenye uhitaji sio tu katika Sekta ya Afya bali hata kwenye elimu na majanga kote Bara na Visiwani.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam - Donatus Richard alisema wameamua kutoa msaada huu kama sehemu ya kutatua changamoto zinazozikabili Sekta ya Afya visiwani humo ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii sehemu ya faida baada ya kodi wanayoipata kila mwaka.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh. Milioni 13 ajili ya kuezekea Kituo cha Afya cha Jang'ombe kilichopo Wilaya ya Mjini Magharibi - visiwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad