HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 14, 2021

SERIKALI YAWAHIMIZA WANANCHI KUHAKIKI USAJILI WA LAINI ZA SIMU ILI KUWA SALAMA MTANDAONI

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (MB) akipokea zawadi kutoka kwa Afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Judith Shao kwenye Banda la Maonesho la Mamlaka hiyo baada ya kupata maelezo ya huduma za Mawasiliano zinazosimamiwa na Mamlaka hiyo. Naibu Waziri Kigahe amesisitiza umuhimu wa wananchi kutumia huduma za Mawasiliano kwa kuzingatia taratibu za usalama mtandaoni.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (MB) akisaini kitabu wakati alipotembelea Banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika Maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (Sabasaba).Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (MB) akipokea maelezo kutoka kwa Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA )Judith Shao juu ya huduma za mawasiliano zinazosimamiwa na Mamlaka hiyo wakati alipotembelea banda la Mamlaka hiyo viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa, Dar es salaam.

Na Mwandishi Wetu
NAIBUWaziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (MB) amesisitiza juu ya umuhimu wa wananchi kupata elimu stahiki juu ya matumizi sahihi ya huduma za Mawasiliano.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati alipotembelea banda la maonesho la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), katika viwanja vya Maonesho ya biashara ya kimataifa, Kigahe amesisitiza kuwa ni muhimu wananchi wakapata elimu ambayo inatolewa na Mamlaka hiyo juu ya matumizi sahihi ya huduma za Mawasiliano.

Kigahe aidha amesisitiza kuwa, ili kutokomeza matukio ya utapeli mtandaoni wananchi hawana budi kushirikiana na Mamlaka hiyo katika kutoa taarifa juu ya matukio ya kitapeli kwenye mtandao, ikiwemo jumbe fupi za kitapeli zinazotumwa kwa watumiaji huduma za Mawasiliano ili kuwalaghai.

Mamlaka ya Mawasiliano ilitoa namba maalum ambayo inamwezesha mtumiaji huduma za Mawasiliano ya simu kutoa taarifa juu ya ujumbe wowote wa kitapeli kwa kuutuma ujumbe huo kwenda namba 15040 ukihusisha namba ya mhusika anaefanya jaribio la utapeli kwa mtumiaji wa huduma za Mawasiliano.

Akiwa kwenye banda hilo Naibu Waziri aidha amepokea maelezo juu ya zoezi la uhakiki wa usajili wa laini za simu kwa mtumiaji huduma za Mawasiliano kwa kutumia namba maalum ya *106# inayomwezesha mtumiaji simu ya mkononi kupata maelekezo ya namna ya kuhakiki namba zilizosajiliwa kwa utambulisho wa namba za kitambulisho cha Taifa, na ikiwa kuna namba ambazo mtumiaji hazitambui anapaswa kuzifuta kupitia kwa wakala wa usajili wa simu anaeiwakilisha kampuni husika ya Mawasiliano.

“Kwa mfano hata mimi laini yangu nimerudia yaani kwenda kuhakiki na kuhakiki tena, tunategemea zile namba za utapeli zisiwe zinatumika tena” alisisitiza Kigahe.

Kigahe aliipongeza TCRA kwa kazi nzuri inayofanya ya kuelimisha umma juu ya matumizi salama ya huduma za Mawasiliano.

Maonesho ya 45 ya biashara ya kimataifa maarufu kama SabaSaba huwakutanisha wafanyabiashara na wajasiriamali mbalimbali wa kitaifa na kimataifa sambamba na taasisi ambazo hupata nafasi ya kuonesha bidhaa na huduma wanazotoa kwa jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad