MISS MWANZA KUMEKUCHA WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 8, 2021

MISS MWANZA KUMEKUCHA WADAU WAOMBWA KUJITOKEZANa Khadija Seif,  Michuzi Tv

SHINDANO la urembo la kumtafuta mrembo wa jiji la Mwanza 'Miss Mwanza' linatarajiwa kuzinduliwa  rasmi Julai 9 mwaka huu Katika ukumbi wa New Mwanza Hotel uliopo katikati ya Jiji la Rock City.

 Akizungumza na Michuzi Tv Muandaaji wa Shindano Hilo Sebastian Kalugulu amewakaribisha wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi na Mashirika mbalimbali kwa kuitikia na kushiriki Uzinduzi huo wa kumsaka mrembo atakayewakilisha vizuri Mwanza.

''Tunakaribisha Mashirika mbalimbali, Kampuni, Taasisi na Wadau mbalimbali kwenye hafla hiyo ya Uzinduzi wa Miss Mwanza na tunategemea Mrembo atakaepatika ataweza kutuwakilisha vyema kwenye mashindano ya Miss Tanzania ikiwezakana Mashindano ya dunia pamoja na kuwa Balozi mzuri kwenye jamii ili vijana wajivunie kuwepo kwa Miss Mwanza." Amesema.

Hata hivyo  Sebastian Kalugulu ameeleza kuwa katika hafla hiyo itaaanza majira ya saa 02:00 usiku ikichagizwa na Burudani mbalimbali huku warembo wenyewe pia wakishiriki kutoa Burudani hizo.

 "Washiriki au Warembo wetu wa Miss Mwanza watashiriki kutoa Burudani pamoja na zulia jekundu kwa ajili ya picha na wageni mbalimbali wataweza kupita ikiwa sehemu ya umoja na kubadilishana mawazo."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad