MSANII wa muziki wa Kizazi kipya Behnam Paul ' Ben Pol' ameachia wimbo wake mpya wenye mahadhi ya Bongo Fleva aliouita ‘Warira’.
Wimbo huu umerekodiwa katika studio za Pizzey records, Mbezi Beach chini ya mtayarishaji mpya aitwaye Chatta kutoka Morogoro.
Akizungumzia ujio wa wimbo huo Ben Pol amesema kuwa tayari wimbo huu unapatikana kupitia mtandao wa YouTube na katika vituo vya radio na TV.
Amesema kuwa hii ni moja ya malengo yake ya kushirikiana na Wasanii au watayarishaji wapya katika kazi zake za mwaka huu.
Ben Pol amewaomba mashabikj wake kuipokea nyimbo yake hiyo mpya ya Warira ili iendelee kufanya vizuri katika soko la muziki.
Ben Pol amesema “ nawapenda sana mashabili wangu wamekuwa na mimi kwa kipindi chote na kila ninapoachia nyimbo mpya wanaupokea na kufanya vizuri kwenye soko la muziki,”
Amesema anawashukuru sana wadau wa muziki kwa sapoti kubwa wanayoendelea kumpatia na naomba wapokee kibao chake kipya ambacho tayari ameshakiachia kwenye vyombo vya habari na You Tube.
Ben Pol ni msanii anayeimba miondoko ya R n B na amekuwa anafanya vizuri katika soko la muziki ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment