HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 17, 2021

WAZIRI WA TEHAMA NA UBUNIFU RWANDA ALITEMBELEA SHIRIKA LA TTCL

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Bakari (aliyesimama) akizungumza kwenye kikao cha pamoja na Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire pamoja na ujumbe alioambatana nao katika ziara yake nchini Tanzania. 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia ziara ya Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire aliyoifanya kwa siku mbili nchini Tanzania kutembelea na kufanya majadiliano na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kituo cha taifa cha kuhifadhi Data (Data Center) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania kutembelea na kufanya majadiliano na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kituo cha taifa cha kuhifadhi Data (Data Center) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire akisaini kitabu cha wageni alipowasili Kituo cha taifa cha kuhifadhi Data (Data Center) kuendelea na ziara yake. Nyuma kutoka kulia ni Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Meja Jenerali Charles Karamba, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba pamoja na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile wakiambatana naye.
Meneja Mkuu wa taasisi ya RURA ya nchini Rwanda, Charles Gahungu (wa pili kushoto) akizungumza katika kikao na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Kulia ni Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Meja Jenerali Charles Karamba na Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire wakifuatilia.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile (katikati) akiwa katika kikao cha pamoja na mgeni wake, Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire (hayupo pichani) pamoja na viongozi wakuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Kituo cha taifa cha kuhifadhi Data (Data Center).
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akizungumza na wanahabari mara baada ya kikao cha majadiliano na Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire pamoja na ujumbe alioambatana nao ambao ni viongozi wakuu wa taasisi zinazo ratibu na kusimamia mawasiliano nchini Rwanda.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amesema nchi za Tanzania na Rwanda zitaendelea kushirikiana na kujengeana uwezo kwenye sekta ya Tehama ili kuhakikisha zinawasaidia wananchi wa pande zote kunufaika kupitia eneo hilo.



Waziri Dk. Ndugulile ameyasema hayo, alipozungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam akiwa katika Ofisi za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), na Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire ambaye amefanya ziara ya siku mbili nchini Tanzania.

Dk. Ndugulile amesema ziara ya Bi. Ingabire inajumuisha kufanya majadiliano na kubadilishana uzoefu katika sekta ya mawasiliano kwa pande zote mbili. Aliongeza kuwa Tanzania na Rwanda ni nchi ambazo zimekuwa na ushirikiano kwa muda mrefu kupitia Shirika la Mawasiliano la Tanzania na lile la Rwanda na mahusiano ya kibiashara.

“TTCL ni moja ya wadau anayepeleka mawasiliano katika nchi ya Rwanda na amekuwa akitoa mawasiliano hayo kwa zaidi ya miaka 10 sasa, hivyo nimemkaribisha Waziri kwanza aje kuona sehemu ambayo mawasiliano yake ya nchi ya Rwanda yanapita na pili kuja kubadilishana uzoefu kwa pande zote mbili.

“..Nchini kwetu hii ni Wizara Mpya (Tehama) na kwa Rwanda kuna hatua ambazo wamepiga katika maendeleo ya Tehama, lakini pia kuja kuangalia fursa zinazopatikana Tanzania na sisi kuangalia fursa hizo kwa nchi ya Rwanda,” alisema Waziri Dk. Ndugulile.

Alisema katika ziara hiyo Waziri wa Rwanda na Tanzania watafanya majadiliano kuangalia maeneo ambayo wanaweza kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuboresha zaidi mahusiano ya pande zote. Sisi kama Wizara ya Teknolojia na Mawasiliano tumefarijika sana kwa ujio wa Mh. Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Ingabire ili sasa kuangalia yale ambayo tumekuwa tukiwasiliana kwa maandishi tuweze kuonana ana kwa ana na hata kujionea uwezo tulionao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akizungumza katika ziara hiyo, alisema ziara ya kiongozi huyo licha ya kudumisha mahusiano baina ya nchi hizo inaendelea pia kukuza mahusiano ya kibiashara kwani TTCL inatoa huduma za internet nchini Rwanda.

Alisema katika ukanda wa Afrika Mashariki nchi ya Rwanda ni miongoni mwa mataifa yaliopiga hatua kubwa kwenye teknolojia (ICT), hivyo ujio wa ziara hiyo ni fursa tosha kwa Tanzania. Alisema katika majadiliano wamekubaliana kuendelea kufanya biashara na nchi hiyo pamoja na maboresho zaidi ya kiushirikiano.

Aidha alibainisha kuwa wamekubaliana kuendelea kubadilishana teknolojia, mafunzo ya kujengeana uwezo, na TTCL inahakikisha inatumia fursa hiyo vizuri ili kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki na Ukanda wa nchi za SADC kutimiza malengo ya Serikali.

Naye Waziri wa Tehama na Ubunifu wa nchi ya Rwamda, Bi. Paula Ingabire akizungumza alisema Rwanda na Tanzania zimekuwa na mahusiano ya kubadilishana teknolojia za kidijitali kwa muda mrefu takribani zaidi ya miaka 10 hivyo ziara hiyo imekuja kuangalia namna ya kuboresha zaidi mahusiano hayo.

Alisema Rwanda licha ya kuwa na mahusiano kibiashara kupitia TTCL imekuwa na utaratibu wa mashirikiano kati ya taasisi za serikali zinazosimamia mawasiliano yaani TCRA kwa Tanzania na RURA kwa Rwanda hivyo ziara yake itaboresha zaidi mahusiano na ushirikiano huo.

Waziri Bi. Paula Ingabire katika ziara hiyo aliongozana na viongozi wakuu wa taasisi zinazo ratibu na kusimamia mawasiliano nchini Rwanda na kutembelea na kufanya majadiliano ya kimkakati na taasisi za TTCL, Kituo cha taifa cha kuhifadhi Data (Data Center) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad