ASAS HALF MARATHON HAPATOSHI IRINGA. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 17, 2021

ASAS HALF MARATHON HAPATOSHI IRINGA.

 
  
Na Khadija Seif, Michuzi Tv
 
KAMPUNI inayotengeneza Maziwa Jiji la Iringa hapa nchini Asas daries limited imeandaa Asas half Marathon kwa ajili ya kueka miili sawa.

Akizungumza na Waandishi Wahabari Dar es salaam Balozi wa Asas daries Haji Manara amesema dhumuni la kueka Asas Half Marathon ni kwa ajili ya kuwakutanisha Wadau mbalimbali na itasindikizwa na burudani mbalimbali .

"Asas half Marathon tunategemea kuanza Agosti 7 mwaka huu yalipo Makao makuu ya Maziwa ya Asas na tunatarajia wakazi wa Iringa na viunga vyake kujitokeza katika hafla hii na watu wengine wanakaribishwa kujiunga nasi."

Steve Nyerere aliongeza kuwa Mbali na Shindano Hilo wakimbiaji watapata fursa ya kutembelea hifadhi kubwa iliyopo Iringa hifadhi ya Ruaha.

"Watanzania nawakaribisha kwenye Shindano hili la Asas half Marathon wajiisajiri kupitia page zetu za Asas na huku zawadi ni nyingi Sana lakini pia tutatembelea hifadhi ya Ruaha ikiwa ni sehemu ya kuthamini vya kwetu na kuvienzi."

Pia amewaomba Wadau wa Michezo kujitokeza kwa wingi kukimbia ili kuweka sawa miili yao pamoja na kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima huku akitaja zawadi ya ng'ombe mkubwa kwa Mshindi wa kwanza.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad