Na Andrew Chale, Zanzibar.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dokta. Hussein Ali
Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mbio za Kimataifa za
Zanzibar zijulikanazo kama Zanzibar International Marathon
zinazotarajiwa kukimbiwa 18 Julai, mwaka huu mjini Unguja zenye lengo la
kukuza uchumi wa bluu.
Waratibu wa mbio hizo wamesema hayo
wakati wa utambulisho rasmi kwa wadau na Wanahabari ambapo walieleza
kuwa, lengo la mashindano hayo ni kukuza na kuchochea Utalii visiwani
humo.
"Lengo la mashindano haya ni kukuza na kuchochea Utalii
visiwani Zanzibar baada ya mtikisiko wa janga la CORONA lililoikumba
Ulimwengu mwishoni mwa mwaka 2019." Alisema Msemaji wa mbio hizo, Hassan
Mssa Ibrahim.
Aidha, alibainisha kuwa, Washiriki wa Marathon
hiyo ni watalii wa ndani na nje, Taasisi, Wanafunzi wa Vyuo vikuu na
wananchi kwa ujumla na yatakuwa endelevu kila mwaka.
"Tunawaomba
Wadau waendelee kutupokea na kujitokeza kwa wingi katika kutuunga mkono.
lengo la mashindano haya ni kukuza na kuchochea Utalii wetu hapa
visiwani.
Katika siku hiyo ya mbio 18 Julai, kutakuwa na mbio za
kuanzia Kilometa: KM 5, KM10, KM 21na pia kutakuwa na mbio maalum za
Watoto za Mita: M 700 huku bingwa wa Marathon akitarajiwa kupata zawadi,
Pia Washiriki wote watapewa zawadi maalum ya Zanzibar kutoka kwa mgeni
rasmi". Alisema Hassan Mussa Ibrahim.
Aliongeza kuwa, Katika mbio
hizo, zenye kauli mbiu; "Tunakuza uchumi wa bluu kupitia michezo
Zanzibar", ambapo sehemu ya mapato yatakayopatikana yanatarajiwa kwenda
kituo cha kuwatunza Wazee Sebleni.
Aidha, Hassan Mussa Ibrahim
alisema washiriki watalipia Tsh. 35000, kwa Watanzania na Wakazi wa
Afrika Mashariki, kwa wageni wa nje watalipia dola USD 50 na Tsh 20000
kwa Wanafunzi wa Vyuo huku kwa watoto watalipia 15000.
"Tayari vituo mbalimbali unaweza kufanya malipo kwa Dar es Salaam ni maduka ya Dauda sports,
Maduka ya Just Fit sports gear Kijitonyama na Mlimani cty.
Kwa
upande wa Zanzibar watalipia kupata ushiriki kupitia CATALUNIA
barbershop, Park Hyatt Zanzibar, Cape Town fish market Zanzibar na
sehemu nyengine zitatangazwa na taratibu zingine kupitia tovuti maalum
ya mashindano". Alimalizia Hassan Mussa Ibrahim.
Katika
utambulisho huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale,
Mhe. Lelant Mussa pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo: Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini, Mhe. Ayou, Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe. Rashid Msaraka,
katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, vijana na michezo,
Kamishna wa Michezo Zanzibar na Wakuu wa Taasisi mbalimbali pia Wadau,
wadhamini pamoja na Mabalozi wa mbio hizo, Zembwela na Maulid Kitenge.
Mgeni rasmi wakati wa utambulisho rasmi wa mbio za Kimataifa za Zanzibar International Marathon, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Lelant Mussa (mwenye kilemba cheusi) akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa mbio hizo pamoja na viongozi wengine na baadhi ya wadhamini.
Awesome and interesting article. Great things you've always shared with us. Thanks. Just continue composing this type of post.
ReplyDelete