
Na Amiri Kilagalila,Njombe
WADAUwa
michezo mkoani Njombe wamesema wanaendelea na jitihada za kutafuta timu
kadhaa zitakazo fanya vema katika mashindano mbali mbali ili kuweza
kurudisha uwakilishi wa mkoa wa huo katika mashindano makubwa ya Ligi
kuu Tanzania.
Hayo
yamebainishwa na wadau mbali mbali wa michezo katika michuano ya ligi
za ngazi ya vijiji, kata na tarafa inayoendelea mkoani humo.
Miongoni
mwa michuano inayoendelea mkoani Njombe ni pamoja na ile ya Mtewele
Super Cup iliyomalizika jana kwa ngazi ya vijiji vya kata ya Uwemba kwa
kuifanya Njomlole Fc kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Uwemba
FC na kujinyakulia zawadi mbali mbali kwa waliofanya vizuri ikiwemo
Kombe,jezi na mipira na hatimaye kuandaliwa kambi kwa ajili vijana
walioonyesha vipawa ili kuendelea na hatua inayofuata.
Diwani
wa Kata ya Uwemba Jactan Mtewele muanzilishi wa ligi ya Mtewele Super
Cup,amesema anatarajia kuona michuano hiyo inaendelea ili kutengeneza
timu itakayovuka ngazi zote za mashindano na kushiriki ligi kuu.
"Tulitafuta
mwalimu toka Songea amekuja hapa ametafuta vipaji na
vimeonekana,Matarajio yetu kuingia ligi ya wilaya,Mkoa na hatimaye Ligi
kuu"Jactan Mtewele diwani kata ya Uwemba.
Ameongeza
kuwa "Sisi baada ya kukamilika kwa michuano hii, tumeandaa wachezaji
watakao ingia kambi maalumu kwaajili ya kuanzisha timu ya kata
itakayohusisha vijiji vyote vya kata ya Uwemba na ndoto kubwa baadaye
ishiriki ligi kuu." Alisema Mtewe
Katika
michuano hiyo mshindi wa wa kwanza amepata kombe,Jezi,pamoja na Mpira
mmoja huku mshindi wa pili akipata jezi pamoja na mpira lakini mshindi
wa tatu akijinyakulia mpra.
Katika
michuano hiyo viongozi wa serikali hawajabaki nyuma ambapo katibu
tawala wa wilaya ya Njombe Emmanuel George kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa
Njombe aliyeshiriki fainali za michuano ya Mtewele Super Cup,Ameagiza
mashindano yanayoendelea mkoani humo yakautangaze vema mkoa.
"Njombe
imekuwa ikitajwa vibaya, Michezo hii itusaidie kubadirika ili sasa
Njombe iwe na sifa nzuri maaana mkoa wetu mara kadhaa umekuwa ukisifika
sana kwa mambo mabaya tu na sio mazuri hii haipendezi." Alisema Emanuel
George
Hata
hivyo swala la afya katika michuano inayoendelea mkoani
Njombe,limeendelea kupewa kipaumbele na kupelekea diwani wa kata ya
Uwemba halmashauri ya mji wa Njombe Ndugu,Jactan Mtewele kukabidhi kadi
31 za bima ya afya CHF iliyoboreshwa kwa vijana 31 walioshiriki kwa
nidhamu katika ligi ya Mtewele Super Cup iliyofika tamati kwenye kata
hiyo.
Sambamba
na jitihada za kimichezo zinazoendelea kwenye kata hiyo,bado wabunge wa
majimbo ya mkoa wa Njombe na wadau wengine wameanzisha ligi mbali mbali
ili kutafuta vipaji vya uwakilishi kuendelea kusaidiana na timu ya
Njombe FC pamoja na Mapinduzi quens zinazoendelea kushiriki michuano ya
ligi za TFF kwa kusua sua.
Awesome and interesting article. Great things you've always shared with us. Thanks. Just continue composing this type of post.
ReplyDelete