Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi
Liberata Mulamula akipokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa
Konseli Mkuu wa Oman mwenye makazi Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi.
Uwasilishwaji wa hati hizo umefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara
jijini Dar es Salaam
Konseli
Mkuu wa Oman mwenye makazi Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi
akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi ndogo za Wizara
jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasilisha nakala ya hati za
utambulisho
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi
Liberata Mulamula akipokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa
Konseli Mkuu wa Msumbiji mwenye makazi Zanzibar Mhe. Agostinho Abacar
Trinta katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi
Liberata Mulamula akizungumza na Konseli Mkuu wa Msumbiji mwenye makazi
Zanzibar Mhe. Agostinho Abacar Trinta katika Ofisi ndogo za Wizara
jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasilisha nakala ya hati za
utambulisho
****************************
Na mwandishi wetu, Dar
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi
Liberata Mulamula apokea nakala ya hati za utambulisho za Makonseli
Wakuu wawili kutoka Msumbiji na Oman wenye makazi Zanzibar.
Makonseli hao ni Mhe. Agustinho Abacar Trinta Konseli Mkuu wa Msumbiji pamoja na Mhe. Said Salim Al Sinawi Konseli Mkuu wa Oman
Pamoja
na mambo mengine, viongozi hao wamedajiliana masuala mbalimbali ya
kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na Kiuchumi baina ya nchi zao na
Tanzania.
Tuesday, June 29, 2021
MAKONSELI WAKUU WA MSUMBIJI NA OMAN WAWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment