HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 29, 2021

Njombe wazidi kupambana kutafuta timu za kushiriki Ligi kuu

 

Na Amiri Kilagalila,Njombe
WADAUwa michezo mkoani Njombe wamesema wanaendelea na jitihada za kutafuta timu kadhaa zitakazo fanya vema katika mashindano mbali mbali ili kuweza kurudisha uwakilishi wa mkoa wa huo katika mashindano makubwa ya Ligi kuu Tanzania.

Hayo yamebainishwa na wadau mbali mbali wa michezo katika michuano ya ligi za ngazi ya vijiji, kata na tarafa inayoendelea mkoani humo.

Miongoni mwa michuano inayoendelea mkoani Njombe ni pamoja na ile ya Mtewele Super Cup iliyomalizika jana kwa ngazi ya vijiji vya kata ya Uwemba kwa kuifanya Njomlole Fc kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Uwemba FC na kujinyakulia zawadi mbali mbali kwa waliofanya vizuri ikiwemo Kombe,jezi na mipira na hatimaye kuandaliwa kambi kwa ajili vijana walioonyesha vipawa ili kuendelea na hatua inayofuata.

Diwani wa Kata ya Uwemba Jactan Mtewele muanzilishi wa ligi ya Mtewele Super Cup,amesema anatarajia kuona michuano hiyo inaendelea ili kutengeneza timu itakayovuka ngazi zote za mashindano na kushiriki ligi kuu.

"Tulitafuta mwalimu toka Songea amekuja hapa ametafuta vipaji na vimeonekana,Matarajio yetu kuingia ligi ya wilaya,Mkoa na hatimaye Ligi kuu"Jactan Mtewele diwani kata ya Uwemba.

Ameongeza kuwa "Sisi baada ya kukamilika kwa michuano hii, tumeandaa wachezaji watakao ingia kambi maalumu kwaajili ya kuanzisha timu ya kata itakayohusisha vijiji vyote vya kata ya Uwemba na ndoto kubwa baadaye ishiriki ligi kuu." Alisema Mtewe

Katika michuano hiyo mshindi wa wa kwanza amepata kombe,Jezi,pamoja na Mpira mmoja huku mshindi wa pili akipata jezi pamoja na mpira lakini mshindi wa tatu akijinyakulia mpra.

Katika michuano hiyo viongozi wa serikali hawajabaki nyuma ambapo katibu tawala wa wilaya ya Njombe Emmanuel George kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe aliyeshiriki fainali za michuano ya Mtewele Super Cup,Ameagiza mashindano yanayoendelea mkoani humo yakautangaze vema mkoa.

"Njombe imekuwa ikitajwa vibaya, Michezo hii itusaidie kubadirika ili sasa Njombe iwe na sifa nzuri maaana mkoa wetu mara kadhaa umekuwa ukisifika sana kwa mambo mabaya tu na sio mazuri hii haipendezi." Alisema Emanuel George

Hata hivyo swala la afya katika michuano inayoendelea mkoani Njombe,limeendelea kupewa kipaumbele na kupelekea diwani wa kata ya Uwemba halmashauri ya mji wa Njombe Ndugu,Jactan Mtewele kukabidhi kadi 31 za bima ya afya CHF iliyoboreshwa kwa vijana 31 walioshiriki kwa nidhamu katika ligi ya Mtewele Super Cup iliyofika tamati kwenye kata hiyo.

Sambamba na jitihada za kimichezo zinazoendelea kwenye kata hiyo,bado wabunge wa majimbo ya mkoa wa Njombe na wadau wengine wameanzisha ligi mbali mbali ili kutafuta vipaji vya uwakilishi kuendelea kusaidiana na timu ya Njombe FC pamoja na Mapinduzi quens zinazoendelea kushiriki michuano ya ligi za TFF kwa kusua sua.

1 comment:

  1. Awesome and interesting article. Great things you've always shared with us. Thanks. Just continue composing this type of post.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad