HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 19, 2021

Equity Bank yatambulisha “Fanikisha Machinga Loan” kwa viongozi wa Masoko na Wafanyabiashara wadogo wa Dar es salaam.

 



Mkurugenzi Mwendeshaaji wa Equity Bank Bi. Esther Kitoka Akimkabidhi zawadi Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto katika Semina  iliyofanyika katika ukumbi wa Golden jubilee. Dar es Salaam Jumamosi 19 Juni 2021
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto akizungumza katika Semina  iliyofanyika katika ukumbi wa Golden jubilee. Dar es Salaam Jumamosi 19 Juni 2021
Mkurugenzi Mwendeshaaji wa Equity Bank Bi. Esther Kitoka Akizungumza katika Semina  iliyofanyika katika ukumbi wa Golden jubilee. Dar es Salaam Jumamosi 19 Juni 2021
Picha ya pamoja na wafanyabiashara wadogo (Machinga)Dar es Salaam Jumamosi 19 Juni 2021
Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Equity Bank. Dar es Salaam Jumamosi 19 Juni 2021



*****************************

Dar es Salaam Jumamosi 19 Juni 2021. Equity Bank Tanzania imeendelea kuonyesha dhamira ya kuwanyanyua kiuchumi wafanyabiashara wadogo maarufu kama Wamachinga kwa kuendesha kongamano kwa viongozi wa Masoko na wafanya biashara zaidi ya 250 jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Golden jubilee, imelenga kutoa mafunzo kwa viongozi hao juu ya mikopo, Bima, na uwekaji wa kumbukumbu za hesabu, ilikusanya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, wakiwemo viongozi wa masoko ya Kariakoo, Feri, Gongo la Mboto, Manzese, Tegeta, Sinza na mengineyo.

Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto, alisema kuwa Serikali mkoani Dar es Salaam inapongeza Benki ya Equity kwa kufanya makongamano ya kuwapa elimu wafanyabishara wadogo ili kuwapa ufahamu wa masuala ya fedha na uwekezaji. “Naupongeza uongozi wa Benki ya Equity, kwa ubunifu huu mliokuja nao wa kuanza kuwakopesha wafanyabishara hawa wadogo kupitia mikopo yenu ya Fanikisha machinga Loans. Jiji la Dar es Salaam linaendelea na juhudi za kurasimisha wafanyabiashara wadogo ili kurasimisha biashara zao na hivyo kuwapa fursa ya kupata huduma kama  vile bima za afya  na huduma za  mifuko ya jamii. Rai yangu kwenu ni kuhakikisha kuwa mikopo hii na fursa nyingine za fedha mnazopewa, zitumike kwa miradi stahiki ili kufanikisha malengo.  Tumieni mikopo hii vizuri na pia mkumbuke kulipa kwa wakati  ili wengine waweze kukopeshwa” alisema Mstahiki Meya.

 

Akizungumza katika warsha hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaaji wa Equity Bank Bi.Esther Kitoka alisema “Benki ya Equity inaendeshwa kwa sera ya kuwawezesha wananchi kwa kuwapatia huduma bora na nafuu za kifedha ili kuweza kuwakomboa kiuchumi. Moja ya kundi ambalo limekuwa likipewa kipaumbele ni kundi la wafanyabiashara wadogo maarafu kama wamachinga. Pamoja na ukubwa wa kundi hili, na ukweli kuwa ndio linaloajiri vijana wengi kuliko kundi lolote, bado limekuwa likibaguliwa na taasisi nyingi za Fedha kwa kisingizio cha kukosa dhamana. Hivyo Benki ya Equity imeingiza sokoni bidhaa ya mikopo iitwayo Fanikisha Machinga loans ikiwa na dhumuni la kutoa mikopo nafuu kwa wafanyabishara wadogo walio katika mijumuiko yao kama masoko na maeneo mengine ya majumuiko. Kwa kuanzia tulianza na wafanyabishara wa masoko ya Kariakoo, Gongo la Mboto na soko la Samaki Feri. Mikopo hii ya Fanikisha, ina lenga kuwakomboa wafanyabiashara hawa kwa kuwapa mikopo nafuu kuanzia shilingi laki moja mpaka milioni moja hadi mbili, kwa kipindi cha miezi mitatu kwa riba nafuu kabisa. Huduma hii pia huwapa wafanyabiashara hao wigo wa kufanya marejesho kwa kipindi cha kati wiki moja hadi mbili ili kuwapa nafasi ya kufanya biashara kwa utulivu” alisema.















  






























No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad