Benki ya UBA yatoa vitabu vya fasihi kwa vituo vya watoto yatima Dar es Salaam - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 20, 2021

Benki ya UBA yatoa vitabu vya fasihi kwa vituo vya watoto yatima Dar es Salaam

 


Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali zaa kuhakikisha kila mtoto kuanzia chekechekea mpaka kidato cha nne wanapata elimu bure, benki ya UBA Tanzania kupitia kitengo cha UBA Foundation umetoa msaada wa vitabu vya fasihi kwa vituo vya watoto yatima vya UMRA na Babu na Bibi vya jijini Dar es Salaam.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu, Muasisi wa kituo cha UMRA Orphanage Center Rahma Juma alisema “Ni muhimu kutambua mchango wa makampuni binafsi kama benki ya UBA Tanzania kwa juhudi za dhati za kuunga mkononi na kuinus sekta ya elimu hapa nchini. Zote tunajua ya kwamba serikali yetu inaongozwa na sera ya serikali ya viwanda. Kwa maana hiyo hatuwezi kuwa na viwanda bila ya kuwa na wasomi wazuri kutoka kwenye jamii yetu, hiyo basi vitabu hivi vitaongeza chachu kwa watoto ambao tunawale hapa kwani wote ni wanafunzi na hivyo kufanya vizuri katika masomo yao na hatimaye kufanikisha ndoto zao pamoja na serikali”.

Rahma aliongeza “nawaomba benki ya UBA na wadau wengine waendelee kutusaidia kwenye nyaja zingine mbali mbali ili kuendelea kutengeneza mazingira bora kwa watoto hawa kujifunza na hivyo kuongeza uelewa na kuwa na taifa lenye ueledi”.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Digitali UBA Tanzania Asupya Bussi“ Sisi benki ya UBA tunaamini jamii iliyoelimika inajengwa kutoka katika watoto pamoja na wanafunzi kuwa na vifaa vya kufundishia vya kutosha hususani vitabu, ili kuwa na maendeleo endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na leo tunathibitisha dhamira yetu kwa kutoa msaada wa vitabu kwa shule hizi”.

Benki ya UBA imekuwa kwa muda mrefu ikisaidia sekta ya elimu hapa nchini kwenye Nyanja mbali mbali. Kwa maana hiyo, uongozi wa benki hii ulianzisha kitengo maalum kijulikanacho kama UBA Foundation kwa ajili ya kuendesha zoezi hili. Na kwa kutimizi hili, tumekuwa tukifanya kazi na serikali na naomba nitoe pongezi za dhati kwani serikali imekuwa ikituunga mkono kwa hili, Asupya alisema huku akiongeza kuwa benki ya UBA itaendelea kusaidia kwenye sekta ya elimu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi wetu.

Tunaamini ya kwamba msaada wa vitabu utachochea ufaulu mzuri kwa wanafunzi katika masomo yao na pia kuongeza ufaulu kwa shule zote hizi, alisema Asupya.

Kwa upande wake, Muasisi wa kituo cha watoto yatima cha Babu na Bibi Apolinary Mutalemwa alisema kuwa msaada wa vitabu hivi umekuja wakati muafaka wakati kituo hicho kilikuwa hakina vitabu kabisa licha ya kuwa watoto wote wanaolelewa hapo na wanafunzi na hivyo tunaahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo".

Aliongeza, watoto wote hawa hapa ni mayatima. Licha ya msaada wa vitabu hivi, lakini kufika kwenu kumekuwa ni faraja sana. Tunatoa pongezi za dhati kwa uongozi wa UBA Tanzania kwa kuamua kuja kututembela. Vitabu hivi vitajenga hali ya kujisomea kwa watoto wetu na kwa vyovyote ufaulu wao kwenye shule utaongezeka, alisema Mutalemwa.

Mkuu wa Kitengo cha digitali kutoka Benk ya UBA, Asupya Bussi Nalingigwa (kulia) akikabidhi vitabu kwa Muasisi wa Kituo cha kulea watoto wanaishi katika mazingira magumu cha Babu na Bibi Apolinary Mutalemwa kwa ajili ya wanafunzi wanaolelewa kituoni hapo. Benki ya UBA Tanzania kupitia UBA Foundation ilitoa vitabu hivyo kwa ajili ya kusaidia watoto kituoni hapo kupata vifaa vya kujisomea.
Mkuu wa Kitengo cha Digitali kutoka benki ya UBA Tanzania Asupya Bussi akiongea na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha watoto yatima cha Babu na Bibi cha jijini Dar es Salaam. Benki ya UBA Tanzania kupitia UBA Foundation ilitoa vitabu vya vituo vya UMRA na Babu na Bibi vyote vya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia watoto kituoni hapo kupata vifaa vya kujisomea.
Mkuu wa Kitengo cha digitali kutoka Benk ya UBA, Asupya Bussi Nalingigwa akikabidhi vitabu kwa Muasisi wa Kituo cha kulea watoto wanaishi katika mazingira magumu (UMRA), Rahma Juma Kishumba kwa ajili ya wanafunzi wanaolelewa kituoni hapo. Benki ya UBA Tanzania kupitia UBA Foundation ilitoa vitabu hivyo kwa ajili ya kusaidia watoto kituoni hapo kupata vifaa vya kujisomea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad