WANAOPOTOSHA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 14, 2021

WANAOPOTOSHA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA


 Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akizungumza kuhusiana naa mikakati mbalimbali ya mawasiliano pamoja na wasambazaji wa taarifa za upotoshaji akiwa katika ziara Mjini Mpanda mkoani Katavi.

* Wanaounda makundi ya kupotosha katika mitandao ya kijamii kukiona cha moto

*Ni kutokana na uzushi wa taarifa zinazolenga kuweka taharuki jamii 


Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv- Katavi 

 NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea amewataka watanzania kutumia mawasiliano kwa ajili ya maendeleo.

Naibu Waziri ameyasema hayo mjini Mpanda mkoani Katavi kutokana na baadhi ya watu wa kuwa wasemaji katika mitandao wakati Msemaji wa Serikali yupo ambaye anaweza kuzungumzia masuala yeyote yanayoendelea nchini.

Kufuatia na kutumika mitandao vibaya Naibu Waziri amesema mikakati ya kuwabaini wanaopotosha kwenye mitandao ya jamii huku akitaka wanaounda makundi kujiandaa hatua zitakazochukuliwa.

Amesema kuna watu katika mitandao ya jamii wamekuwa sehemu ya kuzusha vitu na kutaka watanzania kuvipuuzia.

Amesema kama suala la ugonjwa wizara  afya ipo na ndio wanaweza kuzungumzia ugonjwa.

Amesema mitandao ya kijamii ipo kwa ajili ya kutumika katika maendeleo na sio kuweka taharuki kwa watanzania kwa vitu visivyo na maendeleo.

Naibu Waziri Kundo amesema kuwa kuna mifumo itawekwa ya kuweza kuwabaini watu wanaopika taarifa ikiwemo na watu waundaji wa makundi katika mitandao hiyo.

Amesema mifumo hiyo ikishawekwa Jeshi la Polisi kupitia kwa mkurugenzi wa makosa ya jinai (DCI) watapewa taarifa na hakuna kwa sehemu ya kukimbilia.

Amesema serikali imejenga miundombinu ya mawasiliano katika kuhakikisha wananchi wanapashana habari na sio kufanya watu kufanya vitu ambavyo vinahatarisha jamii.

Naibu Waziri Kundo amesema kuwa watatimiza malengo ya Mh. Rais Dkt.John Magufuli katika kuhakikisha wanasimamia mawasiliano kwa kuleta tija.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad