MAENEO YA PEMBEZONI YAMEKUWA NA MWITIKIO WA INTERNET - NAIBU WAZIRI KUNDO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 14, 2021

MAENEO YA PEMBEZONI YAMEKUWA NA MWITIKIO WA INTERNET - NAIBU WAZIRI KUNDO

 


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akizungumza na Watendaji wa Mkoa wa. Rukwa wakati alipofanya ziara katika Mkoa huo kuangalia hali ya miundombinu ya Mawasiliano kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Carolius Misungu.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akimkabidhi kitabu cha chenye taarifa za ujenzi wa miundombinu ya minara ya Ruzuku ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Winnie Kijazi  wakati alipofanya ziara katika Mkoa huo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Winnie Kijazi alipofanya ziara ya kuangalia hali ya mawasiliano katika Mkoa huo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akizungumza nje ya ofisi za Mkuu Mkoa wa Rukwa kuhusu hali ya mawasiliano katika Mkoa huo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akiangalia bidhaa za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Mkoa wa Rukwa.
Naibu Waziri Kundo akiwa katika kijiji cha Isale kuangalia mnara wa Tigo iliyojengwa kwa Ruzuku ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF.)
Mnara wa Tigo uliojengwa  kwa ruzuku ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF.)

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa Said Mtanda akizungumza katika Kijiji cha Ntuchi wakati Naibu Waziri Kundo Andrea alipofanya ziara katika wilaya hiyo.
Wananchi wa kijiji cha Ntuchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea hayupo pichani.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akiwa na wafanyakazi wa Shirika la Posta pamoja na Watendaji wengine walioko chini ya Wizara hiyo

*Minara yote kujengwa 3G na 4G.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV - Rukwa 

SERIKALI imesema kuwa mwitikio wa matumizi ya data yamekuwa kwa kasi kwa wananchi na kutaka watoa huduma za mawasiliano kujenga miundombinu ili wananchi waweze kutumia katika maendeleo ya kiuchumi.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea wakati wa ziara ya kuangalia hali ya mawasiliano katika Mkoa wa Rukwa, amesema maeneo yaliyokuwa hayana mvuto wa kibiashara ambapo kampuni yalijenga miundombinu ya 2G kwa ajili ya kupiga na kupokea ujumbe sasa maeneo hayo yanahitaji kutumia data na kwenda 3G.

Naibu Waziri Kundo amesema wakati umefika kwa kampuni kujenga miundombinu ya minara yenye mahitaji yote katika dharula kwa maeneo yenye kutumia Nishati ya Jua kuweka Jenereta huku maeneo yaliyopitiwa na Umeme kuunganisha Umeme huo.

Naibu Waziri Kundo amesema kuwa maendeleo hayana Chama amekwenda katika Jimbo ambalo Mbunge wake ni wa Chama cha Demkorasia na Maendeleo (Chadema) kwa kutambua wananchi wanahitaji mawasiliano na sio vyama.

Naibu Waziri huyo alitembelea Vijiji Isale na Ntuchi katika Jimbo la Nkasi Kaskazini kuangalia minara iliyojengwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Tigo kwa ruzuku ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF.)

Amesema minara hiyo Tigo ya Isale na Ntuchi iongezewe uwezo wa 3G katika kipindi kusichozidi miezi miwili ili wananchi hao waweze kunufaika na matumizi ya data.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda ameishukuru ziara ya Naibu Waziri huyo ya kwenda kutatua matatizo ya wananchi.

Amesema kuwa Nkasi ina fursa nyingi za kibiashara hivyo wananchi wanahitaji kupata matumizi ya data ili biashara hizo ziweze kuendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad