HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 2, 2021

WANANCHI TUTHAMINI MIUNDO MBINU INAYOJENGWA NA SERIKALI - MARYPRISCA.

 



Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Wananchi wametakiwa kulinda na kuhifadhi Miundo hasa ya Maji ambayo Serikali imekuwa ikigharamia pesa nyingi kuijenga katika kusogeza Maendeleo na Huduma Nyinginezo za kijamii.

Maji ikiwa Ni hitaji na Huduma ya Msingi katika uhai wa Binadamu Miundo mbinu yake imekuwa ikihujumiwa Mara kwa Mara licha ya Serikali kujitahidi kuwekeza pesa katika Miradi mbalimbali ya hapa Nchini, bado kumekuwepo na Changamoto ya uharibifu na uporaji  wa miundombinu hiyo na hivyo kusababisha kukosekana kwa Huduma ya Maji katika maeneo husika.

Akiwa katika Ziara ya Kikazi Mkoani Kagera ya Kutembelea Kukagua na Miradi ya Maji na changamoto za Maji, Naibu Waziri mwenye dhamana MaryPrisca Mahundi ametembelea na kujionea usanifu wa mradi wa kusambaza Maji wa Kemondo - Maruku unaotekelezwa Halmashauri ya Wilaya Bukoba, ambao upo katika hatua za Awali, na Kisha baadae akatembelea Mradi wa Maji wa Gera Wilayani Missenyi.

Naibu Waziri MaryPrisca amefurahishwa na namna RUWASA kwa Kushirikiana na BUWASA wanavyoendelea kutatua changamoto za Maji kwa Watanzania ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi za Mhe.  Rais Dkt John Pombe Magufuli na  Kampeini yake ya Kumtua Mama Ndio Kichwani.

Katika kuhakikisha adhma ya Rais Magufuli inatimia kwa vitendo, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) wameamua kuanzisha Kampeini ya "Maji Bombani, Bomba Lipi, Bomba Lipo, Bomba la Nyumban."

Kwa upande Mhe. MaryPrisca Ametembelea na kukagua Mradi wa Maji wa Kyaka - Bunazi ambao umefikia 48% na kujionea zinavyoendelea kwa kasi ukiwa Ni msisitizo wa Rais Magufuli alioutoa alipofanya ziara yake  hivi karibuni Mkoani Kagera, akitaja Mradi huo kukamilika kufikia Juni Mwaka Huu.

Pichani linaonekana Tanki la Maji la Mradi wa Maji wa Gera Wilayani Missenyi wenye Thamani ya Shilingi Milioni 570 likiwa tayari limekamilika na Mradi huo umeanza kufanya kazi.
Mmoja Kati ya Wakazi wa Gera akiwa ametwishwa Ndoo ya Maji, akisubiri Naibu Waziri MaryPrisca (Serikali) Kumtua Ndoo hiyo Kichwani Kama Kampeini ya Mhe. Rais Magufuli ilivyo ya Kumtua Ndoo Mama Kichwani na kumsogezea Maji karibu aweze kubeba mikononi kwa umbali mfupi.
Kwa mbali inaonekana sehemu ya Maji ya Mto Kagera ambapo chanzo cha Maji ya Mradi wa Bunazi - Kyaka kinajengwa kwa kasi Sana ili kukamilika kufikia Julai, ambapo Maji hayo yanapandishwa Kilimani kwenye Tanki.
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi MaryPrisca Mahundi (katikati) akiongozana na Msafara wake Kutembelea Mradi wa Maji wa Kemondo - Maruku unaoanza kutekelezwa Eneo la Kemondo Halmashauri ya Wilaya Bukoba.
Muonekano wa Tanki la Mradi wa Maji wa Kyaka - Bunazi lenye Lita za Ujazo 2000m ambalo Kitakuwa linahifadhi Maji ya Wateja Milioni 6.57 limefikia 95% ya Ujenzi wake.

Fundi wanaoendelea na Ujenzi wa Kituo cha kutibu Maji ya Mradi wa Maji wa Kyaka - Bunazi kabla ya Maji hayo kusambazwa kwa wateja, wanaonekana wakiwa kazini wanaoendelea kusuka nondo.
Muonekano wa Jengo la Ofisi za Mradi wa Maji Kyaka - Bunazi likiwa katika hatua hiyo ya Ujenzi wake.

Mhandisi MaryPrisca ambaye ni Naibu Waziri wa Maji akiongea na Wahusika wa Mradi na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati alipofika eneo la Mradi wa Maji wa Kyaka-Bunazi na kujionea shughuli zinazoendelea.

 Naibu Waziri Mhandisi MaryPrisca  akiteta Jambo na Mbunge wa Nkenge Mhe. Florent Kyombo Mara baada ya Ukaguzi wa miradi ya Gera na Kyaka Jimboni Nkenge Wilaya ya Missenyi (picha Zote na Dulla Uwezo)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad