Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdalah Ulega akisoma hotuba yake wakati wa kuzindua mpango mkakati wa maendeleo ya BAKWATA Wilaya ya Mkuranga kipindi cha 2021-2036, ambapo amewapongeza kwa kuanza mapema mpango huo na amewahakikishia yupo pamoja nao kwa kuwaunga mkono mambo mbalimbali.Uzinduzi huo umefanyika leo katika ukumbi wa Flex Kiguza wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani, kushoto ni Sheikh wa Wilaya ya Mkuranga Hamis Mzee.(Picha zote Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv.)
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdalah Ulega akimkabidhi mchango wake Sheikh wa wilaya ya Mkuranga, Hamis Mzee (kulia) baada ya kumaliza kuzindua mpango mkakati wa maendeleo wa BAKWATA Wilaya ya Mkuranga kipindi cha 2021-2036.Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga akizugumza na viongozi wa BAKWATA wilaya ya Mkuranga wakati wa kuzinduwa mpango mkakati wa maendeleo kipindi cha 2021-2036,ambapo amewaomba viongozi hao kuwa ardhi ni mali wasiuze maeneo yao bila ya kufata sheria,kanuni ,utaratibu ili kuepuka kusababisha migogoro na kuendelea kuitunza amani ya nchi yetu.(Picha zote Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv.)
Mkurugenzi wa Wilaya ya mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde akisisitiza jambo. Mkurugenzi wa wilaya ya mkuranga,Mhandisi Mshamu Munde akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga mchango wake katika kuzindua mpango mkakati wa maendeleo BAKWATA Wilaya ya Mkuranga kipindi cha 2021-2036, umefanyika leo katika ukumbi wa Flex Kiguza Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wa BAKWATA Wilaya ya Mkuranga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdalah Ulega.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdalah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa BAKWATA Wilaya ya Mkuranga.(Picha zote Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv.)
No comments:
Post a Comment