*TCRA waelezea maendeleo makubwa ya huduma za Internet Ruvuma.
Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv Songea
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea amesema kuwa Jimbo la Peramiho lina fursa za kibiashara za mawasiliano na kutaka watoa huduma wa kampuni za simu kujenga minara.
Kundo aliysema wakati alipofanya ziara katika Jimbo hilo na kutembelea sehemu zenye changamoto za Mawasiliano katika kijiji vilivyo Kata za Mpitimbi pamoja na Ndokosi
Mhandisi Kundo amesema kuwa kufika katika Jimbo hilo ni kutaka wananchi wafurahie huduma za mawasiliano ambazo katika kufikia asilimia 80 mwaka 2025.
Kundo amesema jimbo la Peramiho linahitaji minara ya 3G na 4G kwa mahitaji ya mawasiliano yamekua na kuhitaji matumizi ya data.
Amesema Rais Dkt.John Pombe Magufuli ameanzisha Wizara ikiwa ni kutaka kutatua matatizo ya mawasiliano.
Kundo amesema kuna miradi mingi ya mawasiliano inayoendelea ni pamoja na mfumo postal code ambapo huduma ya vifurushi zitakuwa kiganjani.
Nae Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John ameeleza namna huduma za mawasiliano ya internet zilivyozidi kuenea mkoani Ruvuma ambapo Wilaya ya Songea peke yake ina jumla ya minara 71 ya mawasiliano ya simu, ikiwepo ya 4G inayopatikana katika baadhi ya maeneo ikiwepo Peramiho, Mpitimbi na Litapwasi.
Mhandisi John amesema huduma ya 4G katika kijiji cha Litapwasi ni ishara kuwa wananchi wa vijijini wanaendelea kuunganishwa kwenye mawasiliano ya data kuelekea kutimizwa lengo la zaidi wa watumiaji wa Internet asilimia 80 ifikapo mwaka 2025.
No comments:
Post a Comment