Wafanyakazi wa Benki ya Equity Tanzania wameungana na wateja wao katika maadhimisho ya ‘Siku ya Wanawake Dunia 2021’. Katika halfa hizo zilizofanyika katika matawi yote ya Benki hiyo nchini, wateja walipata warsa wa kukutana na wafanyakazi na viongozi wa Benki hiyo na kufurahi kwa Pamoja.
Siku ya Wanawake duniani ambayo husherehekewa kila tarehe 8 Machi, ina lengo la kukutanisha wadau mbalimbali ili kutambua mchango wa wanawake na kutatua changamoto zinazowakabili.
to challenge” au “amua kupambana” ikihamasisha uwepo wa usawa wa kijinsia katika jamii na mahali pa kazi.
Akizungumza katika hafla iliyofanyika katika tawi la Mwenge jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Equity Tanzania, Esther Kitoka alisema Benki ya Equity inachukulia kwa umuhimu suala la kumuwezesha mwanamke na ndio maana imeweka bidhaa mahususi na huduma za mikopo nafuu kwa ajili ya kinamama.
“Equity Bank tunatoa bidhaa maalum kwa wanawake kama Eazzy-Kikundi na mikopo nafuu ya Fanikisha tukilenga kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa mwanamke mmoja mmoja kama mjasiliamari au wale walioko kwenye vikundi kama Viccoba na vinginevyo. Nichukue fursa hii kuwakaribisha akina mama wote Equity Bank” alisema.
No comments:
Post a Comment