Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akifurahi wakati wa makabidhiano ya mabati 324 yaliyotolewa msaada na Benki ya Maendeleo TIB kwa ajili ya kusaidia kuezekea vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari Itende, mkoani Mbeya.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wapili kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Paul Ntinika (kulia), Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mhe. Dourmohamed Issa (kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Mahusiano ya Kitaasisi wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella (wapili kulia) wakinyanyua moja ya mabati yaliyotolewa msaada na Benki ya Maendeleo TIB.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wapili kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Paul Ntinika (kulia), Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mhe. Dourmohamed Issa (kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Mahusiano ya Kitaasisi wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella (wapili kulia) wakijiandaa kunyanyua moja ya mabati yaliyotolewa msaada na Benki ya Maendeleo TIB.
Na Mwandishi wetu,
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ambaye pia ni Mbunge wa
Mbeya Mjini amepokea msaada wa mabati 324 kwa ajili ya kusaidia kuezekea
vyumba sita vya madarasa ya Shule ya Sekondari Itende,
mkoani Mbeya ambayo haina shule ya sekondari.
Akikabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa
Mipango, Mikakati na Mahusiano ya Kitaasisi wa Benki ya Maendeleo TIB,
Bw. Patrick Mongella alisema benki hiyo imekabidhi msaada huo kwa
kutambua nafasi yake kama Taasisi ya Maendeleo, ili
kuongeza ustawi wa sekta ya elimu katika Manispaa ya Jiji la Mbeya na
Taifa kwa ujumla.
“Kwa kutambua ukweli kuwa suala la elimu
ni mojawapo ya maeneo tunayoyaunga mkono tuliona ni vyema Taasisi yetu
itoe mchango kwa kuisaidia Manispaa ya Jiji la Mbeya ili kuweza
kukamilisha miundombinu ya elimu kwa wanafunzi wanaochaguliwa
kujiunga na kidato cha kwanza,” alisema Bw. Mongella.
Aliongeza kuwa anaamini msaada huo
utachangia malengo ya Serikali ya kuendelea kuboresha elimu inayotolewa
ili iweze kutoa maarifa na ujuzi wa kutosha kwa wahitimu katika nyanja
zote za elimu hapa nchini.
Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ambaye alikuwa
mgeni rasmi wakati wa makabidhiano hayo alisema kuwa mchango huo unaunga
mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt John Pombe
Joseph Magufuli za kuendeleza kujenga na kukarabati miundombinu ya
elimu ili tunaendelea kuboresha elimu inayotolewa ili iweze kutoa
maarifa na ujuzi wa kutosha kwa wahitimu.
Dkt. Tulia aliishukuru Benki ya Maendeleo
TIB kwa kusaidia kata ya Itende ambayo haina shule ya sekondari kitu
ambacho kinachowalazimu watoto kwenda mbali sana ili kuitafuta elimu
hiyo.
No comments:
Post a Comment