HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 11, 2021

Mwakinyo kuwania mkanda wa Afrika dhidi ya Mzimbabwe, KCB benki yamwaga Sh94.4 million

 

  Mwakinyo kuwania mkanda wa Afrika dhidi ya Mzimbabwe, KCB benki yamwaga Sh94.4 million

Wakati bondia Hassan Mwakinyo atapanda uliongoni Machi 26 kuwania  ubingwa wa Afrika (ABU) wa uzito wa superwelter dhidi ya bondia Mzimbabwe Brendon Denes wa Zimbabwe, benki ya KCB imetangaza kudhamini pambano hilo kwa Sh 94.4 millioni.

Pambano hilo la raundi 12 limepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Nnext Door Arena mwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Jackson Group Sports, Kelvin Twissa.

Twissa alisema  mkanda huo kwa sasa upo wazi na wameamua Mwakinyo kuwania ubingwa huo ili kumwezesha bondia huyo kuingia katika orodha ya viwango vya shirikisho maarufu la ngumi za kulipwa duniani (WBC).

Twissa alisema kuwa Denes mpaka sasa hajapoteza pambano lolote kati ya nane aliyocheza wakati Mwakinyo amecheza mapambano 18 na kupoteza mawili tu.

Alisema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine makali  ambapo bondia Jongo Jongo naye atawania ubingwa wa ABU dhidi ya Olanrewaju Durodora wa Nigeria. Pia bondia Ibrahim Class atapanda ulingoni kumsindikiza Mwakintyo kupambana na bondia ambaye atatangazwa baadaye.

“Hii ni sehemu ya pili ya Rumble In Dar na tunaitarajia kuwa kali na kusisimua kwani mabondia wanaopigana ni moto wa kuotea mbali,” alisema Twissa.

Kwa upande wake,  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB Christine Manyenye alisema kuwa wameamua kutoa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya pambano hili ili kuendeleza mchango wao katika maendeleo ya michezo nchini.

Manyenye alisema kuwa bendi yao pia inadhamini Ligi Kuu ya Tanzania Bara, mashindano ya Ndondo Cup na riadha ambapo ilidhamini mashindano ya Rock City marathon.

“Ni faraja kubwa kwetu kujihusisha na maendeleo ya michezo nchini  ikiwa pamoja na jamii, hivyo tunatarajiamashabiki wa ngumi za kulipwa watajitokeza kwa wingi siku hiyo na mabondia wa Tanzania watashinda,” alisema Manyenye.

Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo alisema kuwa pambano hilo linatarajia kuonekana katika zaidi  ya nchi 30 za bara la Afrika.

Shelukindo alisema kuwa pambano hilo litaonekana kwenye chaneli ya Clouds Plus ambayo ipo kwenye king’amuzi cha DStv na kuwaomba mashabiki wa ngumi za kulipwa kujiunga nacho. Mbali ya benki ya KCB, DStv, pia pambano hilo limedhaminiwa na Onomo Hotel na M-Bet.

Kwa upande wake, Mwakinyo alisema kuwa amejiandaa vyema na pambano hilo na anatarajia kufanya vyema.

“Nipo kwenye maandalizi kwa ajili ya pambano hilo na niatarajia kuendeleza wimbi la ushindi.  Muda uliobakia ni mchache sana ambao nautumia kurekebisha na kuboresha mbinu,” alisema Mwakinyo.


Mkuu wa Masoko wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christine Manyenye (wa pili kulia) akikikabidhi mfano wa hundi kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jackson Group, Kelvin Twissa (wa pili kushoto) kwa ajili ya kudhamini pambano la ubingwa wa Afrika wa super weltwer kati ya bondia Hassan Mwakinyo na Brendon Denes wa Zimbabwe lililopangwa kufanyika Machi 26 kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Masaki. Kushoto ni Baraka Shelukindo wa DStv na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Plus Tv, Ramadhani Bukini.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad