Washindi
wa Pikipiki za miguu mitatu aina ya Lifan Cargo wa Droo ya kwanza ya
Kampeni ya Weka Pesa na Ushinde ‘Bonge la Mpango’ inayoendeshwa na Benki
ya NMB, wamekabidhiwa zawadi zao hizo, huku droo ya pili ya promosheni
hiyo ikiibua washindi wengine 12, wote wakitwaa zawadi zinazofikia
thamani zaidi ya Sh. Mil. 23.
Hafla
Kuu ya makabidhiano hayo ilifanyika NMB Tawi la Gongolamboto, ambako
mkazi wa Kitunda jijini Dar es Salaam, Martha Mmasi, alikabidhiwa
pikipiki yake na Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, huku
hafla kama hiyo ikifanyika Tukuyu - Mbeya kumkabidhi mshindi mwingine.
Akizungumza
kabla ya kumkabidhi Martha pikipiki yake, Donatus alibainisha kuwa NMB
Bonge la Mpango, inalenga kutambua na kuthamini utamaduni chanya wa
wateja kujiwekea akiba, pamoja na kurejesha kwa wateja wake sehemu ya
faida ya benki hiyo ya mwaka uliopita, ambako walipata zaidi ya Sh.
Bilioni 205.
“Wito
wetu kwa wateja wetu, kuchangamkia zawadi tunazozitowa kupitia NMB
Bonge la Mpango, ambazo ni pesa taslimu, pikipiki ya miguu mitatu kama
hii aina ya Lifan, gari dogo ya mizigo aina ya Tata ‘Kirikuu’ na zawadi
kuu ambayo ni gari ya kifahari aina ya Toyota Fortuner yenye thamani ya
Sh. Mil. 169”.Alisema Donatus
Wateja
wa NMB, wanachopaswa kufanya ni kuweka akiba katika akaunti zao kuanzia
100,000, kiasi ambacho kinaweza kuwa kianzio kwa wateja wapya, ili
waweze kuwa sehemu ya wateja wanaowania zawadi ya pesa, pikipiki na
Kirikuu. Pia unapaswa kuwa na akiba ya Sh. Mil. 10 ili kushindania
Toyota Fortuner.
Kwa
upande wake, Martha – mfanyabiashara aliyekiri kuathiriwa kibiashara na
janga la virusi vya corona, lililotikisa toka mwaka jana, alisema
alikua mwenye furaha isiyo na kifani kwa kuibuka mshindi wa pikipiki
hiyo, licha ya kufichua kuwa ujio wa Bonge la Mpango ulimsukuma kuongeza
kasi ya kuweka akiba.
“Kasi
yangu ya kuweka akiba iliongezeka, nashukuru nikajikuta nashinda na
kupitia pikipiki hii, ambayo nakiri kuwa nimeshinda kwa bahati yangu na
sio aina yoyote ya upendeleo, biashara zangu zinaenda kupata nguvu mpya,
kwani itasaidia kuniingizia kipato na kukuza uchumi wangu,” alisema
Martha.
Baada
ya makabidhiano hayo, droo ya pili ilichezeshwa mbele ya Mwakilishi wa
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga, ambapo
washindi 10 wa zawadi ya pesa taslimu kiasi cha Sh. Mil. 3.3
walipatikana, sambamba na washindi wengine wawili wa pikipiki aina ya
Lifan Cargo ambao ni Yusuph Kyando wa Lushoto - Tanga na Rose Mgore wa
Pamba Road Mwanza - jumla kuu ya thamani ya zawadi zao ikifikia Mil. 23.
Zawadi
za wiki za Bonge la Mpango ni pesa taslimu na pikipiki 2 za Lifan
Cargo, wakati zawadi za kila mwezi katika miezi mitatu ya kampeni hiyo
ni gari dogo la mizigo aina ya 'Kirikuu' na zawadi kuu ikiwa ni Toyota
Fortuner itakayotolewa mwishoni mwa kampeni hii.
Mshindi
wa droo ya kwanza ya Kampeni ya NMB Bonge la Mpango Martha Mmasi
akionyesha namba za usajili wa Pikipiki ya Miguu mitatu aina ya Lifan
Cargo baada ya kukabidhiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam,
Donatus Richard (wa pili kutoka kushoto) wakati wa hafla iliyofanyika
katika Tawi la NMB Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Meneja wa Tawi la NMB Airport, Restus Assenga na kulia ni Meneja wa Tawi
la NMB Gongo la Mboto, Demetrius Kagesha.
Mshindi
wa Droo ya kwanza ya Bonge la Mpango Martha Mmasi akijaribu kuendesha
Pikipiki ya Miguu mitatu aina ya Lifan Cargo baada ya kukabidhiwa na
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaan, Donatus Richard (wa pili kutoka
kulia) wakati wa hafla iliyofanyika katika Tawi la NMB Gongo la
Mboto jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa tawi la NMB Airport,
Restus Assenga na kulia ni Meneja wa Tawi la NMB Gongo la Mboto,
Demetrius Kagesha.
No comments:
Post a Comment