HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 3, 2020

DC GONDWE: BOHARI, VIWANDA TUWEKE MAZINGIRA MAZURI KUWALINDA WANANCHI

 

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe amekemea vikali Bohari ya kuhifadhi Kemikali ya Junaco Group Ltd kukosa vigezo na kutofuata Sheria na Taratibu za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Shirika la Viwango nchini (TBS), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tina (TMDA) katika uhafadhi wa Kemikali wa hizo.


DC Gondwe ameyasema hayo wakati wa ziara yake eneo la Bohari hiyo iliyopo Mivinjeni jijini Dar es Salaam, ametoa wito kwa kwa Taasisi hizo kufuatilia Bohari kama hizo kuhakikisha wanafuata Sheria ili kuwalinda Wananchi haswa Wakazi wa eneo hilo la Temeke.


“Wafanyabiashara wa hizi Kemikali kwa kweli hatujui zikikaa vibaya hatuwezi kujua kabisa kama zimeharibiaka au kutoboko wapi, zinaweza kuleta madhara Vipindupindu, na maradhi mbalimbali kwa Jamii”, amesema DC Gondwe.

Kwa upande wake, Meneja wa Kanda ya Mashariki, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Gerald Mollel amesema wamegundua mambo ambayo hayaendani na matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Kemikali nchini, kuchanganya Kemikali hizo sehemu ambazo sio sawa, baadhi ya Kemikali kuisha muda wa matumizi.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe akielekezwa jambo na Meneja wa Kanda ya Mashariki, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Gerald Mollel wakati alipotembelea Bohari ya kuhifadhia Kemikali ya Junaco Group Ltd, eneo la Mivinjeni, Jijini Dar es salaam leo.

Mollel amesema kutokana na uwepo wa Bohari hiyo Kemikali hizo zinaweza kuleta madhara kama kusambaa na kusababisha magonjwa ya Saratani, Vipindupindu na magonjwa ya tumbo.


Naye Afisa Mkaguzi Mwandamizi, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mhandisi Donald Manyama amekiri kuwepo sehemu kubwa ya Kemikali hizo kupitwa na wakati (Expired) lakini zinaendelea kuonekana katika sehemu hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe (kushoto) akisisitiza jambo wakati akitoa maelekezo kwa Afisa wa Bohari ya kuhifadhi Kemikali ya Junaco Group Ltd, Mbwana Guju juu ya uhifadhi wa Kemikali wakati alipotembelea Bohari hiyo, eneo la Mivinjeni, Jijini Dar es salaam leo.

“Walipaswa kufuata taratibu kutengenisha zile zilizoharibika na zile ambazo hazija haribika na kutoa taarifa mapema kwa Mamlaka zinazo husika na usamamizi wa Kemikali, Kemikali nyingine tumepeleka Maabara kufanya utafiti kupata majibu ya haraka”, amesema Manyama.


Mwakilishi wa Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Temeke, Joseph Paul amewataka Wafanyabiashara wanaofanya biashara hizo za Kemikali kufuata na kuzingatia taratibu za nchi ikiwemo kufuata weledi katika kufanya biashara hizo, amezitaka Mamlaka zinazo  fanya ukaguzi kuongeza kasi ya ukaguzi.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe akiingia kwenye Bohari hilo kujionea hali halisi.
Sehemu ya Madumu yaliyohifadhiwa kemikali hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad