HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 3, 2020

KONGAMANO KUIBUA FURSA MPYA ZA BIASHARA YA MAZAO YA BUSTANI KUFANYIKA JIJINI DAR DESEMBA 5

 


WIZARA ya Kilimo kwa kushirikiana na Asasi ya Mazao ya Bustani(TAHA) wameandaa kongamano kubwa la kikanda kwa lengo la kuongeza hamasa ya uwekezaji na kuibua fursa mpya za biashara ya mazao ya bustani nchini ambayo ni matunda, mbogamboga, maua na viungo.

Kongamano hilo litafanyika Jumamosi ya Desemba 5,2020 katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,Mtendaji Mkuu wa TAHA Jacqueline Mkindi amesema itakumbukwa hivi karibuni Rais John Magufuli wakati akilihutubia Bunge la 12 Novemba 13,2020 alianisha vipaumbele kadhaa ili kuimarisha sekta ya kilimo cha mazao ya bustani.

Ametaja baadhi ya vipaumbele hivyo ni kuweka mkazo mkubwa kwenye kilimo cha mazao ya bustani yaani matunda, mbogamboga maua na viungo, katika kuendeleza kilimo cha mazao ya bustani Serikali imekusudia kununua ndege moja ya mizigo ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya bustani, minofu ya samaki na nyama, "Rais alizitaka Wizara ya Kilimo, Biashara na Mambo ya Nje , mabalozi na sekta binafsi kujipanga katika kutafuta masoko na kusaini makubaliano yatakayonufaisha nchi yetu.

"Kama sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli na ili kuhakikisha uwekezaji na upatikanaji wa masoko ya bidhaa na huduma katika tasnia ya kilimo cha mazao ya bustani zinaongezeka; Wizara ya Kilimo inaungana na TAHA kufanya kongamano hilo kubwa la uwekezaji,"amesema.

Amesisitiza kongamano hilo litaongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili kuhakikisha sekta ya kilimo cha mazao ya bustani inaendelea kukua kwa kasi kwa ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi katika kutekeleza vipaumbele vilivyotajwa na Rais Magufuli.

Aidha amesema uwepo wa kanda ya kibiashara za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC) zenye idadi ya watu wapatao milioni 500, inaashiria fursa kubwa ya soko la bidhaa za mazao ya bustani.

"Hii ni fursa kubwa kwa wadau wa sekta binafsi kwa kushirikiana na Serikali kuwekeza katika mnyororo wa thamani wa tasnia ya kilimo cha bustani.Kuwekeza katika mnyororo wa thamani kutafungua fursa mbalimbali za uwekezaji na masoko ya bidhaa za mazao ya bustani,"amesema.
Amesema TAHA inawataarifu tayari baadhi ya washiriki wakubwa wataanza kuwasili kuanzia leo mpaka kesho kutoka Rwanda, Kenya, Sudan, DRC Congo, Comoro na Malawi."Tunatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 400 , wengine zaidi ambao watafuatilia mubashara kupitia mtandao wa kijamii ya TAHA.

"Naomba kuwaarifu watanzania ambao ni wazalishaji ,wafanyabiashara, wasafirishaji , wasindikaji na wadau wengine wakubwa wa horticulture hata kama walishindwa kwa namna moja au nyingine kujisajili kwa muda uliokuwa umepangwa kuhudhuria mkutano huu wa aina yake,"amesema Mkindi. 

Mtendaji Mkuu wa  Asasi ya Mazao ya Bustani (TAHA) Dkt.Jacqueline Mkindi akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu maandalizi ya ufunguzi wa Kongamano kubwa la Kikanda lenye lengo la kuongeza hamasa ya uwekezaji na kuibua fursa mpya za biashara ya mazao ya bustani nchini ambayo matunda,mbogamboga,maua na viungo.Kongamano hilo ambalo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa,litafanyika Jumamosi,Desemba 5,2020 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad